tag:blogger.com,1999:blog-55386274062571538492024-03-13T10:27:01.587+03:00BONGOJAMII Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comBlogger3091125tag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-14461521328915361502018-05-05T08:16:00.001+03:002018-05-05T08:16:56.541+03:00Bora ule sumu kuliko kula hela ya serikali – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa kula hela za serikali ni sawa na kula sumu kwahiyo ni bora ule sumu kuliko kula hela ya serikali.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Mkoa Morogoro katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kidatu – Ifakara mkoani Morogoro amesema kuwa haiwezekani ahaingikie kukusanya hela kutoka kwa wananchi masikini alafu wanakula.

“Kuna baadhi ya miradi makandarasi wamekula pesa, nataka kuwahakikishia hao wakandarasi wamekula sumu, hela za serikali haziliwi, ni nafuu ukale sumu kuliko kula hela za serikali ya awamu ya tano.Haiwezekani mimi nihangaike kukusanya hela kutoka kwa wananchi masikini, halafu unapewa kandarasi we uende kuila, nataka kuwaeleza wakandarasi mmekula wa chuya,” amesema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais Magufuli alimpigia simu live, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Kitila Mkumbo mbele ya wananchi wa kijiji cha Kidodi Morogoro kutaka kumchukulia hatua mkandarasi aliyepewa kutekeleza mradi wa maji wa kijiji hicho, ambaye alishapewa pesa za mradi milioni 800 na maji hayajafika kwa wananchi.Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/17521960100203508996noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-19358690221442703952017-09-19T10:40:00.008+03:002017-09-19T10:40:56.895+03:00HUENDA UCHAGUZI KENYA UTASOGEZWA MBELE

Uchaguzi mpya wa urais nchini Kenya huenda ukaahirishwa kutoka tarehe 17 mwezi ujao. Tume ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC, imekuwa ikikutana kuangalia uwezekano wa kuahirisha Uchaguzi huu baada ya kampuni ya Ufaransa ya Safran Morpho kuomba muda zaidi kuboresha mitambo inayotumiwa kuwatambua wapiga kura.

Mbali na hilo, Muungano wa Upinzani Nasa, unaoongozwa na Raila Odinga, umesema Uchaguzi hautafanyika iwapo marekebisho hayatafanyika ndani ya Tume ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Ezra Chiloba Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo.

Chama cha Jubilee cha rais Uhuru Kenyatta kinashutumu shinikizo hilo la upinzani na kusisitiza uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-86952041986371766042017-09-19T10:40:00.003+03:002017-09-19T10:40:11.830+03:00MBUNGE CHADEMA KUPELEKA HOJA BUNGENI ,MUDA WA URAIS UPUNGUZWE

Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA) John Heche amefunguka na kusema anakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi ili kupunguza muda wa viongozi kukaa madarakani kutoka miaka mitano na iwe miaka minnee kama Marekani.

John Heche amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii zikiwa zimepita siku kadhaa toka Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia (CCM) kusema anatarajiwa kuwasilisha muswada binafsi bungeni kulitaka bunge kufanya marekebisho ya katiba ili viongozi waweze kukaa miaka saba. Jambo ambalo Heche anapinga na kusema kuwa muda ambao viongozi wanakaa madarakani ni mkubwa sana.

"Nakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi kupunguza muda wa kukaa madarakani kwa Rais, wabunge na madiwani kutoka miaka 5 mpaka 4 tuwe kama Marekani ili kutoa nafasi kwa wananchi kuwa na maamuzi zaidi kuhusu uendeshaji wa nchi yao" Alisema John Heche

Aidha John Heche amesema kuwa kiongozi akikaa madarakani muda mrefu anajisahau na kuona ile nafasi kama ni yake pekee yake jambo ambalo si sawa hata kidogo

"ukikaa sana madarakani unafikiri nchi ni mali yako, kuna viongozi wengi sana wazuri ila hawajapata muda tu wa kuongoza" alisisitiza John Heche.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-41943613533539018632017-09-19T10:40:00.002+03:002017-09-19T10:40:00.220+03:00SABABU ZA UTETEZI WA MANJI KUSOGEZWA MPAKA SEPT 25

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, 'imepiga kalenda' kusikiliza ushahidi wa utetezi wa kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili mfanyabiashara Yusufally Manji.

Kesi hiyo 'imepigwa kalenda' baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis kuwa na udhuru wa kikazi na Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Cyprian Mkeha anayeisikiliza kuridhia ombi la Jamhuri.

Vitalis alidai jana kesi hiyo, ilipangwa kuendelea na ushahidi wa utetezi, lakini amepata udhuru wa kikazi na kuomba tarehe nyingine ya kuendelea.

Hakimu alisema kesi hiyo itasikilizwa mfululizo kuanzia Jumatatu mpaka Jumatano ijayo.

Kabla ya kupangwa tarehe nyingine ya kusikiliza kesi hiyo, hakimu alimuonya Manji kwa kuchelewa kufika mahakamani kusikiliza kesi yake.

Manji alidai kuwa aliwasiliana na wakili wake kwasababu alikwenda hospitali na kwamba tukio hilo halitajirudia tena.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa kati ya Februari 6 na 9, mwaka huu eneo la Upanga Sea View, jijini Dar es Salaam, Manji alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-23286050329514269262017-09-19T10:40:00.001+03:002017-09-19T10:40:01.290+03:00MKURUGENZI TANESCO ALIMWA BARUA YA KUJIELEZA

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani amemtaka Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk Tito Mwinuka kuandika barua kujieleza ni kwa nini ameshindwa kuanza ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Kigamboni.

Dk Kalemani ametoa agizo hilo baada ya kutembelea vituo vya kupoozea umeme vya Gongo la Mboto, Kurasini na Kigamboni.

Mwezi uliopita naibu waziri alimwagiza Dk Mwinuka kuanza ujenzi haraka lakini baada ya kutembelea jana Jumatatu amekuta eneo hilo bado halijafanyiwa usafi.

“Nataka kesho( leo) nipate taarifa ya maandishi ni kwa nini hadi sasa hujaanza ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Kigamboni licha ya kukuagiza uanze ujenzi,” aliagiza.

Dk Kalemani alisema Agosti alitembelea eneo hilo na kumuagiza mkurugenzi kujenga uzio ili watu wasivamie eneo hilo.

Alisema pia, alimuagiza kuanza ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme kwa sababu Sh5 bilioni zimeshatengwa kwa kazi hiyo.

“Nashangaa sasa ni mwezi mmoja lakini hakuna kilichofanyika, umeshindwa hata kufyeka majani ili kuonyesha kuna mradi utafanyika hapa,” alihoji Dk Kalemani.

Naibu waziri aliagiza makandarasi kwenye vituo vya kupoozea umeme kumaliza kazi kwa wakati ili kuondoa matatizo ya umeme kwa wakazi wa Mbagala, Kigamboni na Gongo la Mboto.

“Sitalala nitakuwa natembelea miradi hii kila mara hadi itakapokamilika,” alisema.

Akizungumzia agizo hilo, Dk Mwinuka alisema tangu naibu waziri alipolitoa wamekuwa wakifuatilia kibali cha athari za mazingira ambacho hutolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc).

“Tukipata kibali tutaanza ujenzi mara moja na tunakuahidi kazi hiyo itamalizika kwa muda uliopangwa Machi mwakani.

Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile alisema kuchelewa kukamilika kwa vituo vya kupoozea na kusambaza umeme kunasababisha matatizo ya nishati isiyo ya uhakika katika jimbo hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa alisema mradi huo ukianza atausimamia kwa kuwa tatizo la umeme linaathiri maendeleo na uchumi.

“Kila siku napokea ujumbe wa maandishi wa simu kunijulisha tatizo la umeme, ni aibu kwa kuwa wakati mwingine nashindwa nijibu nini,” alisema.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-81938787432961908512017-09-19T10:40:00.000+03:002017-09-19T10:40:06.199+03:00WATU 7 WASHIKILIWA NA POLISI KWA MAUAJI YA WANAWAKE KWA IMANI ZA USHIRIKINA

Na Tiganya Vincent -RS –TABORA
WATU saba wa kijiji cha Mwambondo wilayani Uyui wanashirikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwauunguza kwa moto wanawake wanne wakiwatuhumu kuwa wachawi na wanahusika na kifo cha mume wa mmoja wao.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa alizozipata kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo Wilbroad Mtafungwa.

Alisema kuwa chanzo cha vitendo hivyo vya kinyama zilianzia baada ya Mtu mmoja aliyekuwa akiitwa Mafumba Jirawisi kufariki kwa sababu ya maradhi lakini baadhi ya watu walianza kumtuhumu mke wa marehemu anayeitwa Manugwa Lutema kuhusika na kifo cha mume wake na kuamua kumpeleka porini na kuanza kumshambulia huku wakitaka awaeleze watu wanaoshirikiana naye kuwafanya vitendo vya kichawi.

Mwanri alisema kuwa mama huyo baada ya kupiga sana na kuumia aliamua kutaja ovyo majina ya majirani zake na ndipo nao wakaunganishwa naye na kuendelea kupigwa na kuunguzwa katika sehemu za siri.

Kufuatia vitendo hivyo vya kinyama Mkuu huyo wa Mkoa amemwagiza kuwasaka watu waliobaki ambao wamehusika katika kitendo hicho wakiwemo Makamanda wa sungusungu ili hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Mmoja wa majeruhi wa tukio hilo la kinyama alisema kuwa alilazimika kutaja majirani zake ili kutaka kunusu roho yake baada ya kuona mashambulizi yanazidi na anasikia maumivu makali.

Kwa upande wa ndugu wa waathiri wameomba wagonjwa wao watibiwe bure kwa sababu tukio hilo limetokea wakati wakiwa hawana kitu na hawajiandaa na kutokuwa na fedha ya kulipia matibabu

Akijibu ombi la ndugu hao Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunin Kamba alisema wagonjwa wote waliojeruhiwa na kuuguzwa moto watapewa matibabu kwa mkopo katika Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa ya Kitete ,malipo yatafanyika baadaye.

Alisema kuwa lengo ni kutaka kwanza kuokoa maisha yao kutokana na unyama waliofanyiwa na kundi hilo la watu.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kitete Dkt.Nassor Kaponta alisema kuwa wanaendelea kuwapatia huduma katika Hospitali hiyo na hakuna majeruhi ambaye atahamishiwa kwingine kwa sababu wanauwezo wa kuwasaidia wakiwa katika eneo hilo hilo.

Aliwataja waliojeruhiwa ni Maria Sahani , Elizabeth Kashindye, Manugwa Lutema na Raheli Mikomangwa.

Kabla ya kufariki marehemu ambaye alikuwa mganga wa kienyeji alikwenda kutoa matibabu kijiji cha jirani na baada ya kurejesha akaanza kuumwa na hatimaye usiku wake alifariki kwa sababu ya ugonjwa.

Vitendo vya kinyama ikiwemo mauaji kwa wanawake Mkoani Tabora vinaanza kuonekana kama vya kawaida ambapo mapema mwezi Agosti mwaka huu wilayani Nzega wakinamama watano walipoteza maisha baada ya kushambuliwa na kisha kuchomwa moto na mwezi huo huo wilayani Sikonge mtu mmoja alinusurika kifo baada ya kufungiwa nyumbani kwake na nyuma kuwahwa moto

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-66826863784123095332017-09-18T13:49:00.001+03:002017-09-18T13:49:34.489+03:00VIDEO : MSIGWA NA LEMA WAFUNGUKA MAZITO WALIPOHOJIWA NAIROBI KUHUSU TUNDU LISSU

Wabunge wawili wa Chadema wametumia mahojiano nje ya nchi kuzungumzia matatizo ya Tanzania wakisema hayawezi kumalizwa na mtu mmoja bali kwa mifumo imara ya mihimili ya Mahakama, Bunge na Serikali.

Wakizungumza katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha KTN cha Nairobi, Kenya jana Jumapili walisisitiza umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya ili kuipa nguvu mihimili hiyo.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema ufisadi ambao Rais John Magufuli anaushughulikia sasa ulifanywa na watendaji waliokuwa chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Alisema chama hicho kimeongoza nchi tangu Tanzania ilipopata Uhuru, hivyo ufisadi huo ulifanywa na viongozi waliokuwa chini ya chama hicho.

“Ili tuwe na mfumo wenye nguvu tunatakiwa kubadilisha Katiba ili tuwe na Mahakama na Bunge huru,” alisema.

Lema alisema kumtegemea mtu mmoja hakuwezi kuleta mafanikio kama ambayo yamefikiwa na Kenya.

Alisema Katiba ikibadilishwa na kuwa na vipengele mbalimbali, vikiwemo vya kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na kumshtaki Rais akitoka madarakani Tanzania itakuwa imepiga hatua.

Alisema mabadiliko ya Katiba nchini Kenya si tu yataisaidia katika siasa bali katika kukuza uchumi wao.

“Uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Kenya kufuta matokeo ya Rais si tu yatawasaidia kisiasa bali yatajenga imani hata kwa wawekezaji,” alisema.

Alisema wawekezaji wataongezeka nchini Kenya kwa sababu wanakuwa na imani na Mahakama.

Kwa upande wake, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alisema Rais ana nguvu kuliko mihimili mingine na amekuwa akitoa maelekezo kwa mihimili hiyo.

“Bunge la Tanzania limetekwa na Serikali, wenzetu CCM wako wengi kuliko sisi wapinzani, wakikaa kwenye Party Caucus (vikao vya chama) yao wanaamua mambo yenye manufaa kwa chama chao,” alisema.

Alisema madhara ya wabunge wa CCM kufanya uamuzi wenye manufaa kwa chama hayawaathiri wapinzani tu, bali Watanzania kwa jumla.

Wabunge hao wako jijini Nairobi kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Nairobi baada ya kupigwa risasi Septemba 7 mwaka huu akiwa nyumbani kwake Area D, mjini Dodoma.

==>Wasikilize hapo chini

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-83563519705109797542017-09-18T13:48:00.003+03:002017-09-18T13:48:10.786+03:00WATU 13 WAPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI

Watanzania 13 wamefariki na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la biashara Lubanda takribani kilomita 80 kufika kituo cha polisi cha Fika salama karibu na Mto Katonga wilaya ya Mpigi huko Kampala, Uganda.

Ajali hiyo imehusisha gari aina ya fuso yenye namba za usajili UAH 970P na coaster yenye namba T540 DLC waliokuwa wakitumia watu hao wakiwemo watanzania ambao inasemekana walikuwa wakitoka kwenye harusi ya binti wa Dkt. Annette Ibingira ambaye ni mke wa mhazini wa shule ya Wazazi ya Kampala nchini Uganda Dkt. Ibingira.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Nkozi pamoja na Double Cure Clinic zilizopo nchini Uganda huku miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo imepelekwa hospitali ya Gombe kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi nchini humo.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-4667353907842276192017-09-18T13:48:00.002+03:002017-09-18T13:48:02.003+03:00UPELELEZI KESI YA KABURU NA AVEVA WAKAMILIKA

Upelelezi wa awali katika kesi ya utakatishaji fesha inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa leo September 18, 2017 kuwa, upelelezi wa awali wa kesi hiyo umekamilika ambapo jalada la kesi limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili alisome na kueleza kama anaona umekamilika au la.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi September 27, 2017.

Aveva na Kaburu wanashtakiwa na TAKUKURU wakikabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba na kutakatisha fedha kiasi cha dola za Marekani 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.

Upelelezi uliokuwa unafanyiwa kazi ni nyaraka za kughushi maandiko zilizokuwa zimepelekwa kwa mtaalam kufanyiwa uchunguzi ili kubaini makosa hayo.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-452664598897109152017-09-18T13:48:00.001+03:002017-09-18T13:48:01.605+03:00MJAMZITO ACHOMWA MKUKI , WAWILI WACHOMWA MOTO

Watu watatu wameuawa kwenye Bonde la Yaeda Chini katika matukio tofauti, ikiwamo wawili kuteketezwa kwa moto, huku mjamzito akichomwa mkuki.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga alisema jana kuwa matukio hayo yalitokea juzi kwenye vijiji vya Dumanga na Mongo wa mono vilivyopo katika Bonde la Yaeda Chini.

Mofuga alisema katika tukio la kwanza watu watatu waliodaiwa kuwa majambazi walipora pikipiki na wakati wanakimbia mmoja aliyejulikana kwa jina la Makafo Elia alishindwa kukimbia akakamatwa na wananchi baada ya mafuta ya pikipiki kwisha na wananchi hao kumuua kwa kumchoma moto na kuteketea hadi kuwa majivu.

Alisema katika tukio la pili Martin Boay (25) alimchoma mkuki mjamzito Elizabeth Elias (35) na kufariki dunia, lakini naye aliuawa na wananchi wenye hasira walioamua kumfunga mikono na miguu na kumtupa kwenye moto ambako aliungua hadi kubakia majivu. “Hadi hivi sasa bado polisi wanaendelea na uchunguzi wa matukio hayo matatu ili kuhakikisha mambo ya kujichukulia sheria mkononi yanakomeshwa,” alisema Mofuga.

Aliongeza kuwa kamati ya ulinzi na usalama imekemea tabia ya watu kujichukulia sheria mikononi. Pia, mkuu huyo wa wilaya amemuagiza mkuu wa polisi wa wilaya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika ili iwe fundisho kwa wengine.

“Bonde la Yaeda Chini lina historia ya matukio ya uhalifu hasa mauaji, ujangili wa nyara za Serikali na wizi wa mifugo. Tunaanzisha harambee kwa kuhamasisha wananchi na wadau wengine ili kujenga kituo cha polisi katika bonde hilo,” alisema.

Mofuga aliongeza kuwa, ujenzi wa kituo na nyumba za familia 12 utagharimu Sh435 milioni na unatakiwa kuanza mara moja.

Alisema ameanza harakati za kuwaomba wadau, wananchi na Serikali kuchangia ujenzi huo ili kutafuta amani ya kudumu katika eneo hilo.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-21957219818626209042017-09-18T13:48:00.000+03:002017-09-18T13:48:03.677+03:00ZITTO KABWE AANIKA HADHARANI ALICHOAMBIWA NA LISSU HOSPITALI

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kudai amerudi nchini akiwa na unyenyekevu mkubwa zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri alioonyeshwa na Mbunge Tundu Lissu pindi alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Zitto ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa facebook asubuhi ya leo na kusema japo Lissu ameumizwa sana lakini hakuacha kumuonyesha ucheshi licha ya kuwa na maumivu makali aliyokuwa nayo katika mwili wake.

"Siku mbili hizi nilizoenda kumuona Lissu zimeniacha nikiwa mawazo sana, nimerudi nchini nikiwa kwenye unyenyekevu zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri ambao ndugu yangu amenionesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali. Siyo mara nyingi hapa nchini kusikia tukiongelea ujasiri lakini namfikiria lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi, najua hivyo ndivyo alivyo", ameandika Zitto.

Pamoja na hayo, Zitto ameendelea kwa kusema "waliomshambulia wamemuumiza kweli na bado wakati tuliokuwa naye amenionesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri, alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu siyo kitu rahisi kwa mtu yeyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha niumie moyo kama asingesema maneno haya kwangu kuwa 'tumeshinda. Tumeshashinda", amesisitiza Zitto.

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa kwenda jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyopata, ambapo mpaka sasa yuko huko kwa matibabu.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-54833267160407500092017-09-18T11:08:00.001+03:002017-09-18T11:08:29.147+03:00FAMILIA YA LISSU KUKUTANA KWENYE KIKAO KIZITO

Shangazi yake Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, Ninaa Sawa(kushoto) akiwa na mama mdogo wa Lissu, Bula Muro nyumbani kwa wazazi wa Mbunge huyo Mahambe, Ikungi Singida. Picha zote na Herieth Makwetta.

Siku 10 baada ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi, familia yake imezungumzia tukio na kusema mwishoni mwa mwezi huu watafanya kikao Dar es Salaam wajue nini cha kufanya.

Baba mdogo wa Lissu, Muro Sawa (79), alisema kitu ambacho wazazi wangefurahia ni kumwona kijana wao akirudi nyumbani akiwa mzima.

“Familia tutakaa kikao kushauriana ili tujue suala hili tunalitatua vipi, lakini niiombe Serikali kumzidishia ulinzi kijana wangu. Sisi familia tuna uchungu mkubwa kuhusu hili,” alisema Sawa.

Shangazi wa Lissu, Ninaa Sawa Muro (83) alisema, “Tunakula chakula hakishuki, matonge yanakaba shingoni, maungo yote yanauma kwa sababu ya mtoto wetu, tangu siku ile niliposikia nilikuwa kwenye kiti ghafla nikaanguka na kuanza kutetemeka.”

Alisema alijisikia vibaya baada ya kuambiwa na mtoto wake taarifa hizo, “Aliniuliza umesikia kwamba Tundu Lissu amepigwa risasi? Nikanyamaza, nikaona joto. Kwa jinsi shangazi yangu anavyonipenda hata anikute Manyoni hata Dar es Salaam ananiita jina langu la kikwetu anakuja ananikumbatia iliniuma sana.”

“Alifanywa hivyo kwa nini? Kama tunavyojiona wote roho moja tumfikirie huyo Tundu Lissu,” alisema shangazi huyo ambaye baada ya baba yake Lissu kuzaliwa ndiye aliyemfuata.

Mama mdogo wa Lissu, Bula Muro, alisema baada ya kupata taarifa alianguka chini na kuanza kulia hakufikiria kama amepona.

Mitandao ilivyoiliza familia

Mmoja wa wanafamilia, Msengi Ntandu Mughwai alisema walipata shida siku hiyo ya tukio, “Tulipanga kwenda Dodoma wakasema turudi anaendelea na matibabu, tulihisi wanatudanganya sababu mtandaoni wanasema hali mbaya na kwa kuwa walikuwa ni wanafamilia waliotushauri, tuliamua kurudi usiku kwa kweli kesho yake kulikuwa na habari za ajabu kwenye mitandao yaani zilituumiza sana,” alisema.

Msengi alisema walikuwa wakipigiwa simu na kupewa taarifa zenye utata na wakiingia mitandaoni wanaona habari za ajabuajabu na kwamba hali kwao ilikuwa mbaya.

“Kwa kweli tulipata shida, wazazi wetu walikuwa wanakuja mara kwa mara tunawajibu kwamba anaendelea vizuri lakini wazee wetu walikuwa wanapata taarifa mbaya kwingine kutokana na mitandao ya kijamii,” alisema.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-65888382193733415092017-09-18T11:06:00.000+03:002017-09-18T11:06:18.368+03:00WANAFUNZI 16,000 HATARINI KUKOSA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

WAKATI mwezi mmoja umebaki kabla ya mwaka mpya wa masomo kuanza kwa vyuo vikuu nchini,

Wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 16,000 kati ya 61,000 walioomba kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wako hatarini kuikosa hata kabla ya zoezi hilo kuanza kutokana na taarifa za maombi yao kuwa na dosari.

Hata hivyo, uongozi wa juu wa bodi hiyo umesema wanafunzi hao bado wana nafasi ya kurekebisha taarifa zao licha ya dirisha la kutuma maombi kufungwa Jumatatu iliyopita.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul–Razaq Badru, akizungumza na Nipashe kwa simu jana, alisema hadi siku ya mwisho ya maombi Septemba 11, wanafunzi wanaokadiriwa kuwa 61,000 walikuwa wametuma maombi ya kupewa mkopo kutoka bodi hiyo kwa mwaka ujao wa masomo 2017/18 utakaoanza Novemba.

Alisema kati yao, wanafunzi 16,000 walikuwa na dosari ndogondogo zilizoonekana katika maombi yao, huku wanafunzi wapatao 45,000 wakiwa wamekamilisha vizuri taarifa za maombi hayo.

"Wanafunzi hao bado wanaruhusiwa kurekebisha taarifa zao kwa sababu maombi hufanyika katika mtandao. Bodi bado inafanya uchambuzi wa taarifa," alisema Badru.

Mkurugenzi huyo alizitaja dosari ambazo zimeonekana kwa wanafunzi wengi waliotuma maombi ya mkopo kuwa ni pamoja na kutokuambatanisha vyeti, kuambatanisha cheti ambacho hakijahakikiwa, baadhi ya barua za vyeti vya kifo kutohakikiwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita).

Alisema bodi hiyo bado inaendelea na uchambuzi wa taarifa za wanafunzi hadi Oktoba 2 utakapokamilika na majina ya waliopangiwa vyuo yatakuwa yameshatolewa.

Badru alisema wanafunzi ambao fomu zao zimebainika kuwa na matatizo, hutumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) na kutakiwa kurekebisha.

Aliongeza kuwa Oktoba 10 majina ya wanafunzi waliopangiwa mikopo yatakuwa yameshafahamika.

Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Tahliso), kupitia kwa Mwenyekiti wake, Stanslaus Kadugalize, ilitoa ombi jana kwa HESLB kutoa nafasi kwa wale wote waliokosea kujaza fomu hizo, ili wafanye marekebisho yanayotakiwa.

"Inawezekana waliojaza vibaya fomu hizo wanatoka katika mazingira magumu ya maisha kiasi cha kushindwa hata kumudu matumizi ya kimtandao," alisema.

"Ili kuepuka kuwaacha walengwa, Tahliso tunaiomba Heslb iliangalie suala hilo kwa jicho la pili, ili kuwapa nafasi kwa mara nyingine."

Alisema kuna uwezekano mkubwa wanafunzi waliokosea kujaza fomu hizo ndio wenye uhitaji mkubwa kuliko waliopatia ujazaji wa fomu hizo.

WENGI WATAKOSA
Mei 13, akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, mjumbe wa kamati hiyo, Hussein Bashe, aliliambia Bunge wamebaini wanafunzi wengi watakosa mkopo wa elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2017/18 licha ya kuwa na ufaulu mzuri.

Alisema mwaka jana (2016/17), wanafunzi 48,502 walijaza fomu kwa ukamilifu, lakini 25,555 tu ndiyo walipata mikopo na hivyo kuacha wengine 22,947 wakiwa hawana mikopo kutokana na bajeti iliyotengwa ya Sh. bilioni 427.5 kutotosheleza mahitaji.

Bashe ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), alisema mwaka 2017/18, HESLB imeombewa bajeti ya Sh. bilioni 427.5 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi (sawa na bajeti ya mwaka 2016/17) ilhali ufaulu wa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita umeongezeka kutoka asilimia 88 mwaka 2012 hadi asilimia 99 mwaka huu.

"Kamati inaona kwamba, suala la elimu ya juu ni haki ya msingi kwa watu wenye sifa," Bashe alisema, "katika mwaka ujao wa fedha, wanafunzi wengi zaidi watakosa mikopo licha ya ufaulu wao mzuri.

"Kamati inashauri serikali kuongeza bajeti ya HESLB, ili wanafunzi wengi zaidi wanaostahili waweze kupata mikopo kwa maendeleo ya taifa letu."

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-65434313109066894192017-09-18T10:59:00.003+03:002017-09-18T11:02:02.081+03:00BRAZIL YAISAMEHE TANZANIA DENI LA BILLION 445

Serikali ya Brazil imeisamehe Tanzania deni Dola 203milioni ambazo sawa Bilioni 445 ambalo limetokana na mkopo uliotolewa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979.

Balozi wa Tanzania Nchini Brazil Dk Emmanuel Nchimbi amesaini mkataba huo kwaniaba ya Tanzania huku Wakili wa Hazina ya Taifa Dk Sonia Portella Nunes akisaini kwa niaba ya Serikali ya Brazil.

Balozi Nchimbi ameishukuru Serikali ya Brazil kwa msamaha huo ambao amesema umeunga mkono jitihada za Rais Dk. John Magufuli kujenga uchumi imara wa Tanzania.

Balozi Nchimbi pia ameuhakikishia Serikali ya Brazil utayari wa Tanzania katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uchumi na Brazil.

Hivyo kuanzia sasa kampuni za Brazil zinaruhusiwa kukopa katika Benki za Brazil kwa ajili ya kutekeleza miradi nchini Tanzania lakini pia Serikali ya Tanzania inaruhusiwa kuanzisha majadiliano ya miradi mipya ya maendeleo.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-53944724419822393732017-09-18T10:59:00.002+03:002017-09-18T10:59:03.999+03:00POLISI WAMKAMATA MBUNGE MSUKUMA GEITA

Polisi mkoani Geita wanamshikilia Mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku (Musukuma) kutokana na vurugu zilizotokea eneo la mgodi wa GGM Septemba 14 mwaka huu.

Mbunge Msukuma na madiwani wa wilaya ya Geita walifunga barabara zinazoingia kwenye mgodi wa GGM wakishinikiza kulipwa dola 12 milion zinazotokana na kodi ya huduma.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Mponjoli Mwabulambo jana alithibitishwa kukamatwa kwa Msukuma na kusema askari walimkamata katika eneo la CCM mjini Geita.

Kamanda amesema kukamatwa kwa Musukuma ni mwendelezo wa Polisi kuwakamata watu wote waliohusika katika vurugu zilizotokea Septemba 14.

Amesema tayari wamekamata madiwani wengine wawili na wananchi watano na kwamba jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi na msako wa kuwakamata wote walioshiriki.

“Bado tunaendelea na msako na hawa ni wahalifu kama wahalifu wengine na sheria lazima ichukue mkondo wake na Musukuma tumemkamata sio kwamba amekuja mwenyewe ”amesema

Kamanda amesema kwa sasa wanaendelea na mahojiano na wakikamilisha sheria itachukua mkondo wake na kwamba kosa la jina halina kikomo na wote walioshiriki vurugu za kufunga barabara lazima wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria .

Hadi sasa jeshi la polisi mkoani Geita linawashikilia madiwani kumi wa halmashauri za wilaya ya Geita waliofunga barabara zinazoingia mgodi wa GGM na kuharibu miundo mbinu ya maji yaliyotengenezwa na GGM kwa ajili ya shughuli za mgodi na wananchi wa mji wa Geita katika kijiji cha Nungwe jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Mgogoro wa madiwani na GGM

Madiwani wa halmashauri mbili za wilaya ya Geita juzi walifunga barabara za kuingia katika mgodi wa dhahabu wa GGM wakishinikiza kulipwa dola 12milion zinazotokana na ushuru wa huduma kuanzia mwaka 2004 hadi 2013.

Madiwani hao wanadai fedha hizo ni haki yao kwa mujibu wa sheria kwasababu mgodi ulipaswa kulipa ushuru wa huduma wa 0.03 toka mwaka 2004 hadi 2013 na hawakulipa na badala yake walilipa dola 200,000 kwa kipindi chote kinyume na sheria.

Msimamo huo wa madiwani unapingwa na uongozi wa mgodi wanaodai kuwa mgogoro uliopo unasababishwa na kupingana kwa sheria ambazo zote zimetungwa na bunge.

Meneja mawasiliano ya jamii Manase Ndoroma amesema sheria ya madini iliwaruhusu kulipa dola 200,000 kwa mwaka huku sheria ya baraza la madiwani ikiwa imepitisha malipo ya 0.3 jambo ambalo limesababisha mgogoro na kwamba suluhisho pekee ni kwenda mahakamani.

Tayari serikali mkoani hapa imewataka madiwani hao kuwa watulivu na kumsubiri Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, pamoja na kamishna wa madini kufika mkoani hapa leo Jumatatu kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-21533929370235702932017-09-18T10:59:00.001+03:002017-09-18T10:59:04.384+03:00POLISI YAFAFANUA SAKATA LA WATOTO WATATU KUPOTEZA MAISHA KWENYE MLIPUKO WA BOMU ARUSHA

Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amewataka viongozi waliopo karibu na kambi za mazoezi ya kijeshi kuweka utaratibu wa kuwakumbusha wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona vitu wasivyovijua hasa vyenye asili ya chuma ili kuepusha madhara.

Kamanda Mkumbo ametoa hadhari hiyo alipokuwa akizungumzia tukio la vifo vya watoto watatu wakazi wa kata ya Loksale wilayani Monduli vilivyosababishwa na mlipuko wa bomu walilookota wakati wanachunga mifugo na kuanza kulichezea kama mpira ambalo lililipuka na kuwajeruhi vibaya miguuni.

Akizungumza kwa njia ya simu kamanda Mkumbo amesema licha ya kuwa tukio hilo ni la bahati mbaya lakini lingeweza kuepukika kama watoto hao wangeweza kutoa taarifa ya kitu walichokiona.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa watoto hao wangeweza kufanya hivyo kama wangekuwa wanakumbushwa na wazazi wao mara kwa mara wanapokwenda machungani.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Monduli Bw. Iddy Kimanta aliyezungumza na ITV kwa njia ya Simu amesema watoto hao wote ni wanafunzi wa shule ya msingi Nafko na wawili akiwemo Landisi Setabau miaka 12 na Samweli Nyandusi miaka 9 walikuwa wanasoma darasa la kwanza wakati mwingine aliyetajwa kwa jina la Seuri Losila miaka alikuwa darasa la tatu.

Viongozi wa eneo lililopotokea tukio hilo wamesema kimsingi tukio hilo ni bahati mbaya kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakielimishwa juu ya kufuata maelekezo na mara nyingi wamekuwa wakitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja kutoa taarifa wanapoona mabaki ya vyuma.

Kwa mujibu wa viongozi hao katika maeneo mengi ya wafugaji wakati wa likizo watoto huwasaidia wazazi wao kuchunga mifugo na pia wakati wote wamekuwa wakitoa taarifa wanapokutana na vitu kama hivyo na wahusika wamekuwa wakifika mara moja na kuvichukua.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-23338353377832382172017-09-18T10:59:00.000+03:002017-09-18T10:59:05.481+03:00POLISI WAWILI WAHUKUMIWA MIAKA 35 JELA

Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu askari Polisi wawili wa kutoka kituo cha Oysterbay jijini Dar es Salaam na watu wengine sita kwenda jela miaka 35 kwa makosa mawili ya kukutwa nyara za serikali na kujihusisha na mtandao wa ujangili.

Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali, Salimu Msemo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, ambapo aliwataja polisi hao wa zamani waliokutwa na hatia ni wenye namba D 8656 CPL Senga Nyembo na G 553 PC Issa Mtama washtakiwa walikutwa na meno 70 ya tembo yenye thamani ya Sh. milioni 800.

Wengine sita waliokuwa nao wote wamekutwa na hatia ni pamoja na Prosper Maleto, Seif Mdumuka, Amri Bakari, Said Mdumuka, Ramadhan Athuman na Musa Mohamed.

Aidha, amesema kuwa washtakiwa hao walikutwa na kosa hilo katika eneo la kituo cha ukaguzi cha Kauzeni lililopo Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani kabla ya kufikishwa kortini na kukumbana na adhabu hiyo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa katika kosa la kwanza, washtakiwa walihukumiwa kwenda jela miaka 20 kila mmoja na faini kwa kila mmoja, wakati katika kosa la pili, washtakiwa wawili ambao ni hao polisi, walihukumiwa miaka 15 kwenda jela.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-20591542513715821572017-09-18T08:09:00.001+03:002017-09-18T08:09:20.640+03:00HABARI ZILIZOPEWA UZITO WA JUU KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA18

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-36500668205260585472017-09-17T21:38:00.007+03:002017-09-17T21:38:44.617+03:00 Okwi atupia 2, Bocco 1, Mambo yalikuwa hivi Simba Vs Mwadui Fc

SIMBA SC imewapa burudani ya nafsi mashabiki wake leo baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Nyota wa mchezo wa leo kwa mara nyingine amekuwa mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi aliyefunga mabao mawili na kufikisha mabao matano katika mechi mbili tu za Ligi Kuu alizocheza msimu huu, kufuatia kufunga mabao matatu katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa kwanza.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa Emmanuel Mwandembwa, aliyesaidiwa na Joseph Masija na Michael Mkongwa, hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao hilo lilifungwa dakika ya saba na Okwi aliyekosa mchezo uliopita wa Simba ikitoa sare ya 0-0 na Azam Jumamosi iliyopita Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kutokana na kuchelewa kurejea baada ya kwenda kuichezea timu yake ya taifa, Uganda dhidi ya Misri mechi ya kufuzu Kombe la Dunia mwakani Urusi.

Okwi alifunga bao hilo kwa shuti la umbali wa mita 25 baada ya kumchungulia kipa wa Mwadui, Arnold Massawe aliyekuwa amesogea mbele kidogo kufuatia pasi ya winga Shiza Kichuya aliyekuwa anacheza kama kiungo zaidi leo.

Mwadui pamoja na kumiliki vizuri mpira walipopata nafasi, lakini hawakuwa na mipango kabisa ya kuipenya ngome imara ya Simba chini ya mabeki wa timu za taifa za Uganda na Tanzania, Juuko Murshid na Salim Mbonde.

Kipindi cha pili nyota ya Simba iliendelea kung’ara na dakika ya 67, Okwi tena akawainua vitini mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kwa kufunga la pili kwa shuti la umbali wa mita zisizopungua 20 baada ya pasi ya beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Mashabiki wa Simba walizomea mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mcamroon, Joseph Marius Omog mara mbili kwanza akimtoa Mghana Nicholaus Gyan na kumuingiza Mwinyi Kazimoto dakika ya 61 na baadaye akimtoa Kichuya na kumuingiza Mrundi, Laudit Mavugo dakika ya 65 wakionekana kabisa kutaka mshambuliaji John Bocco ndiye atolewe.

Bocco akawaonyesha mashabiki wa Simba kwamba Omog alikuwa sahihi katika mabadiliko yake kwa kufunga bao la tatu dakika ya 72 kwa shuti la umbali wa mita 20 na zaidi pia.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-60964203538136116042017-09-17T21:38:00.003+03:002017-09-17T21:38:10.564+03:00CHANZO CHA MOTO KWENYE NYUMBA YA ZITTO CHAANIKWA HADHARANI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema kuongezeka joto katika betri za sola ndio chanzo cha moto uliounguza Nyumba ya Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe jana jioni.

Nyumba hiyo ipo mtaa wa Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga katika wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.

Amesema joto hilo limesababisha mlipuko wa moto kwenye betri za sola na hivyo nyumba kushika moto na kuteketea yote.

Polisi wanamshikilia mlinzi wa nyumba hiyo, Norbert Joseph kwa mahojiano zaidi ili kubaini kama kuna uzembe wowote uliofanywa na kusababisha moto kuwaka.

Msaidizi wa Zitto anayeifahamika kwa jina la Nyembo Mustafa ametaja thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo kwamba ni Sh 45 milioni.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-66616063287006393082017-09-17T21:38:00.002+03:002017-09-17T21:38:07.335+03:00RC MAKONDA ATANGAZA NEEMA HII KWA WATUMISHI WA DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza mpango kabambe wa kuwasaidia watumishi wa umma kutokana na kazi ngumu wanazozifanya za kulitumikia taifa la Tanzania.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam RC Makonda ameeleza kuwa watumishi wa kada za elimu, afya na ulinzi wanafanya kazi kubwa mpaka inafikia hatua wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa makazi yao.

Hivyo RC Makonda kupitia wadau amefanikisha hilo ambapo watumishi wa umma kwenye kada tatu tajwa hapo juu wataweza kuuziwa kiwanja kwa kiasi cha shilingi 4000 kwa kipimo cha square meter moja na watapewa hati ya umiliki wa kiwanja.

"Kwa kawaida square meter moja ya kiwanja huuzwa shilingi 15000 hivyo watumishi hawa watauziwa kwa kiasi cha shilingi 4000 na watalipa kwa muda wa miaka mitano pindi watakapo ingia makubaliano" Alisema RC Makonda.

RC Makonda ameeleza kuwa mpango huo kabambe utanufaisha takribani watumishi elfu thelasini na saba (37,000) huku akieleza kuwa tayari watumishi 700 wameanza kunufaika na mpango huo.

RC Makonda amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli itaendelea kuboresha maisha ya watumishi wa umma kwani wanamchango mkubwa kwa taifa.

" Mpango huu ni rahisi sana yaani kiwanja cha milioni tatu mpaka tano unaweza kulipa taratibu kwa muda wa miaka mitano" Alisisitiza RC Makonda.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-77424115191782055122017-09-17T21:38:00.001+03:002017-09-17T21:38:10.224+03:00BAVICHA WATANGAZA SIKU RASMI YA KUSOMA ALBADILI

Baraza la Vijana wa CHADEMA wilayani Muheza mkoani Tanga wamekanusha kusoma albadili ambayo walidhamiria kuifanya siku chache zilizopita, wakisema bado wanalipa muda huku mtaani kukiwa na tetesi kuwa ilishasomwa.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television mwenyekiti wa BAVICHA Muheza, Joseph Saja, amesema sababu ya zoezi hilo kutofanyika ni kwamba siku walizotangaza kuwataka waliofanya tukio hilo kujisalimisha zilikuwa hazijaisha, hivyo wataendelea na zoezi hilo mapema wiki ijayo.

"Siku ambazo tuliwapa wale watu kujitokeza ilikuwa mwisho Ijumaa, na mpaka leo bado hawajajitokeza sasa ndio tutatekeleza majukumu yetu ya kuanza kwenda huko tunakoenda kuisoma, inawezakana katika juma tatu au jumanne ndio tutatoka kwenda", amesema Joseph Saja.

Wiki iliyopita BAVICHA wilayani Muheza mkoani Tanga walitangaza kusoma albadili ili kuwajua watu waliomshambulia kwa risasi Tundu Lissu, na kuisaidia serikali ambayo mpaka sasa haijafahamu waliohusika.

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-45863961108176777452017-09-17T21:38:00.000+03:002017-09-17T21:38:09.355+03:00MKUU WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI APATA AJALI

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Pwani (SSP) Abdi Issango amelazwa kwenye Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Kibaha Mkoani Pwani baada ya kupata ajali.

Kamanda huyo amepata ajali Septemba 16, saa kumi jioni Kijiji cha Kibiki Wilaya ya kipolisi ya Chalinze mkoani humo akiwa na familia yake ambapo baba yake mzazi alifariki papohapo.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Jonathan Shanna amemtaja marehemu kwamba anaitwa Hamis Issango, huku akisema mama yake mzazi alijeruhiwa vibaya huku ndugu yake mmoja akipoteza maisha.

"Ajali imesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi wanne akiwemo Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani na aliyefariki ni baba yake’’alisema

Pia amesema majeruhi wengine ni mdogo wake ambaye ni mwanafunzi hao wote wamelazwa kwenye Hospital ya Tumbi.

Amesema kamanda huyo alikuwa akisafiri na familia yake hiyo kutokea Singida kuelekea Kibaha na waliligonga kwa nyuma lori lillokuwa limeharibika barabarani.

Kamanda shanna amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa lori aliyeshindwa kuweka alama za kuashiria gari lake ni bovu alilokuwa ameliegesha pembezoni mwa barabara.

Kamanda Shanna amesema dereva wa lori hilo na utingo wake walikimbia polisi wanaendelea kuwatafuta.

Chanzo: mwananchi

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-30191636280959348962017-09-17T14:29:00.003+03:002017-09-17T14:29:00.144+03:00NYALANDU AWEKA HADHARANI ALICHOONGEA NA LISSU HOSPITALI NAIROBI

Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Lazaro Nyalandu amesema amezungumza na Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ambaye ameonyesha uso wa tabasamu, huku akimshukuru Mungu kwa kumruhusu kuwa hai.

Nyalandu katika ukurasa wake wa Facebook ameandika, “Muda mfupi uliopita, nimeonana na Mh. #TunduLissu katika chumba chake Hospitali ya Nairobi na kuzungumza naye kuhusu hali yake na anavyoendelea.”

“Ukweli ni kwamba, ameumizwa vibaya. Imeelezwa kwamba madaktari wanaendelea na hatua kadhaa za matibabu, wakiwa wameanza kwa kumuimarisha (stabilization), ili kuufanya mwili uweze kumudu hatua zaidi za utibabu anazopaswa kufanyiwa,” amesema Nyalandu.

Amesema anaamini hatua zaidi na za haraka zitahitajika kumsaidia apate huduma za kitabibu katika ubora na ufanisi uliopo kwa sasa duniani.

“Ni maombi yangu kwetu sote, tuweke pembeni tofauti zetu za kiitikadi, ama mitazamo, tuungane na kushikamana kama Taifa kwa ajili ya kumwomba Mungu anyooshe mkono wake na kumponya,” amesema Nyalandu.

Nyalandu amesema, “Sote tuungane kutoa msaada wa hali na mali kwa kadri ya uhitaji wake. Amani iwe naye!”

Lissu anaendelea na matibabu hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.

Mwananchi:

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-5538627406257153849.post-42803181650834245662017-09-17T14:29:00.002+03:002017-09-17T14:29:01.363+03:00POLISI YAKAMATA WATANO KWA KURATIBU MAOMBEZI YA TUNDU LISSU

Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam, linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kuratibu shughuli za maombezi maalum kwa ajili ya mbunge Tundu Lissu, katika viwanja vya TIP Sinza.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Murilo Jumanne aliyekuwa eneo la tukio, amesema wameamua kuwakamata watu hao kwa kuwa wanatishia amani na utulivu wa nchi.

"Wale wenye nia mbaya ambao bila shaka wana ajenda binafsi ajenda ambazo kimsingi zina uelekeo wa kutishia masuala ya amani, mimi kama Kamnda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, siwezi kukubali hali hiyo itokee kwenye eneo langu, watu wanaendelea na shughuli zao na wachache wakiwa wamevaa nguo za kawaida lakini wameficha tishirt ndani, wanafika sehemu wanaanza kuzitoa", amesema Kamanda Jumanne.

Kamanda Jumanne ameendelea kwa kuwataka wananchi kuacha kufanya mikusanyiko ya aina hiyo, na iwapo wanahitaji kufanya ibada waende kwenye sehemu za ibada.

Jana Jeshi la polisi Kanda maalum lilitoa taarifa ya kupiga marufuku kusanyiko lolote lisilo halali kumuombea Mbunge Tundu Lissu ambaye yuko Nairobi kwa matibabu, na kusema ni kuhatarisha hali ya aman

Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/03158026874713476330noreply@blogger.com