SIMBA SC YASITISHA MAANDAMANO WALIYOPANGA KUFANYA | BONGOJAMII

SIMBA SC YASITISHA MAANDAMANO WALIYOPANGA KUFANYA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Rais wa klabu ya Simba baada ya kushauriana na kamati ya utendaji ya klabu,imeamua kusitisha maandamano iliyopanga kuyafanya Jumanne ijayo, baada ya nia na dhamira njema ya serikali kutaka kushughulikia sintofahamu inayoendelea baina ya klabu na Shirikisho la Soka nchi (TFF).

Ikumbukwe jana klabu yetu kupitia kwenye barua iliosainiwa na Rais wetu Evans Aveva, iliandika kwa Jeshi la Polisi nchini ikiomba kibali cha maandamano ya amani, yaliyopangwa kuhudhuriwa na viongozi,wanachama na washabiki wa klabu, kwenda Wizara inayosimamia Michezo nchini, ili kupeleleka kilio chetu juu ya TFF.

Kwa namna inavyoshughulikia malalamiko ya muda mrefu na ya sasa ya klabu hii kubwa nchini.
Katika barua ilioandikwa na katibu Mkuu wa Baraza la michezo nchini (BMT), Kwa niaba ya Serikali,imetutaka Shirikisho na Klabu kutafuta namna sahihi na iliyo na weledi katika kushughulikia changamoto hizi zinazoweza kuvuruga amani ya nchi. 

Serikali kupitia barua hiyo,imeahidi pia kutukutanisha pande zote haraka iwezekanavyo,ili kwa pamoja tumalize sintofahamu hii. Klabu ya Simba haina mashaka yoyote na Serikali na vyombo vyake, hivyo inaamini itaitisha kwa uharaka mkutano huo muhimu kwa maslahi ya pande zote mbili na mchezo wa Soka kwa ujumla.

Tunawaomba wanachama na washabiki wetu watulie na sote tuache majibizano yoyote ili kutoa fursa kwa Serikali kusimamia kikamilifu jambo hili na kwa sasa tunafanya taratibu na Jeshi la Polisi nchini kuwajulisha kusudio letu la kusitisha maandamano hayo.

IMETOLEWA NA… Haji S Manara
Mkuu wa Habari wa Simba Sc

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts