TETESI ZA KUONDOKA KWA WAYNE ROONEY MSIMU HUU HIZI APA | BONGOJAMII

TETESI ZA KUONDOKA KWA WAYNE ROONEY MSIMU HUU HIZI APA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Nahodha wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney amesema kuwa ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ndiye aliyevujisha siri, kwamba Rooney hana raha na anaona ni wakati mwafaka kwake kuondoka Old Trafford kwa kuwa hapati nafasi ya kucheza.

Jose Mourinho ambaye ni kocha wa United anaonyesha kutomuweka Rooney kama chaguo la kwanza lakini mara kadhaa, naye amekuwa akiumia.

Rooney ambaye ameichezea Man United kwa miaka 13 tokea alipojiunga nayo akiwa kinda kutoka Everton, amekuwa akiandamwa na mamumivu ambayo pia yamechangia akose mechi kadhaa.

Imeelezwa, hana uhakika pia kucheza mechi ijayo ya Man United ambayo itakuwa ya Europa League dhidi ya Anderlecht na itapigwa nchini Ubelgiji, Ahamisi.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts