HUYU APA REFA ATAKAYE CHEZESHA MECHI YA SIMBA VS MBAO | BONGOJAMII

HUYU APA REFA ATAKAYE CHEZESHA MECHI YA SIMBA VS MBAO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya michuano ya Azam Sports Federation Cup HD msimu wa 2016/17, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limemteua Ahmed Kikumbo wa Dodoma kuwa mwamuzi wa mchezo wa fainali kati ya Simba SC na Mbao SC utakaofanyika Uwanja wa Jamburi Mei 27, 2017 kuanzia saa 10.00 jioni.


Kikumbo atasaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba ni Florence Zablon pia wa Dodoma wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Peter Temu wa Arusha. 


TFF inazitakia timu zote, Simba, Mbao, Waamuzi pamoja na Kamishna wao pamoja na wanafamilia wa mpira wa miguu, mchezo mzuri wenye fanaka kwa kila upande.


Alfred Lucas Mapunda


Ofisa Habari na Mawasiliano TFF

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts