FLOYD MAYWEATHER AMPA KICHAPO MC GREGOR KATIKA PAMBANO LA NDONDI | BONGOJAMII

FLOYD MAYWEATHER AMPA KICHAPO MC GREGOR KATIKA PAMBANO LA NDONDI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Mchuano mkali wa ndondi kati ya Conor McGregor na mwanandondi Floyd Mayweather Jnr umemalizika huko Las Vegas, Nevada nchini Marekani, baada ya kuchelewa kuanza kwa muda wa saa moja hivi.

Floyd Mayweather Jnr ameibuka mshindi katika mchuano huo.

Maelfu ya watu wamefika katika mji wa Las Vegas katika jimbo la Nevada nchini Marekani, kutizama mchuano huo mkali wa ndondi, unaofanyika leo Jumapili.

Masumbwi hayo yalikuwa ya raundi kumi. Awali wachanganuzi walisema kuwa Floyd Mayweather Jnr alikuwa ameanza kulemewa katika raundi tatu za mwanzo na mpinzani wake, kabla ya kujizoazoa na kuanza kumrushia makonde mazito mazito Conor McGregor, ambaye alionekana kulemewa hasa kuanzia raundi ya saba.

Alishindwa kuhimili makonde mazito ya Maywheather na kushindwa kumaliza raundi ya 10.

Tayari McGregor ambaye amechana chale mwilini, ni bingwa wa taji la Ultimate Fighting- mchezo ambao mwanandondi anatumia mbinu zote za upiganaji, akitumia makonde na mateke.

Lakini nyota huyo wa miaka 29, hawajawahi kushiriki mchuano wa makonde ya kulipwa- Huku May-weather menye umri wa miaka 40 akitajwa kuwa mpinzani wake hatari zaidi katika masumbwi.

May-weather, anapigiwa upatu wa kushinda mchuano huo, huku akiahidiwa dola milioni 100, ilihali mpinzani wake McGregor, akiahidiwa Dola milioni 30.

Dola milioni 600 zinatazamiwa kupatikana kutokana na mauzo ya moja kwa moja ya tiketi ya kutizama makabiliano hayo ya ndondi. Ambayo pia inatizamwa na mamilioni ya watu moja kwa moja kwenye Runinga huku wengine wengi wakifuatilia katika mitandao.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts