WEMA SEPETU ARUSHA JIWE GIZANI | BONGOJAMII

WEMA SEPETU ARUSHA JIWE GIZANI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Malkia wa filamu Bongo , Wema Abraham Sepetu ametupa jiwe gizani ambalo bado halijajulikana ni kwenda kwa mtu gani na kumwambia bado wa kumshusha hajazaliwa kwani yeye alivyo ni majaaliwa kutoka kwa maulana na siyo kujitakia.

Wema ametupa jiwe hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kusema kuna mtu kamuharibia siku hivyo na kumwambia kwamba yeye hakujitakia kuwa alivyo hivyo mtu huyo ajue kutofautisha.
"Wa kunizima hajazaliwa bado jamani... Alafu mjue kutofautisha kati ya Kujaaliwa na kujitakia... Alhamdulillah nyingi kwa Maulana wangu... Sikujitakia... Ni majaaliwa tu... To whom it may Concern... Kuna mtu kajua kuniharibia siku wallah... " Wema Sepetu.


Dongo la Wema mtandaoni
Aidha Wema ameongeza kwa kusema katu hawezi kujitutumua kwani anaogopa kujiumiza.
Vilevile tukio hilo linaunganishwa moja kwa moja na mtu ambaye Wema Sepetu amemuhisi anataka kujaribu kudukua mtandao wake wa Instagram hali iliyompelekea kumuandikia ujumbe kuwa katu hatamuweza hivyo awe mpole.



Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts