MAJINA YA WALIOKUWA WAMEFAULU KATIKA USAILI WA AJIRA SERIKALINI , KUFUTWA | BONGOJAMII

MAJINA YA WALIOKUWA WAMEFAULU KATIKA USAILI WA AJIRA SERIKALINI , KUFUTWA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Watu wote waliokuwa wamefanya usaili kwa ajili ya ajira serikalini kupitia Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma kabla ya ajira kusimamishwa, watafutwa ndani ya miezi 6 na kulazimika kuomba upya kipindi ajira hizo zitakapotangazwa tena.

Hilo limebainishwa na sekretarieti hiyo kupitia majibu kwa wadau mbalimbali kwa mwezi Desemba ambao wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa kila mwezi kupitia tovuti yake, na kubainisha kuwa suala hilo litawahusu wale ambao walifaulu usaili lakini kabla hawajapangiwa vituo vya kazi au kupewa barua na waajiri wao, ajira zikasimamishwa ili kupisha uhakiki wa watumishi hewa.


Taarifa hiyo imesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa sekretarieti hiyo, kwamba majina ya waliofaulu huhifadhiwa kwenye kanzi data (Database) kwa muda usiozidi miezi sita, na baada ya hapo majina hayo hufutwa.


"Kwa mujibu wa Taratibu zetu za uendeshaji wa mchakato wa ajira majina ya waombaji kazi waliofaulu lakini hawakupangiwa vituo vya kazi kwa sasa huhifadhiwa kwenye kanzi data kwa muda usiozidi miezi sita"Imesema taarifa hiyo


Swali lingine kutoka kwa mdau na jibu lake liko kama ifuatavyo:-


Kwa kuwa ajira zilisitishwa mwezi Juni, na sasa ni mwezi Desemba, utaratibu huo unamaanisha kuwa wasailiwa wote waliofaulu lakini hawakupangiwa kazi, watalazimika kusubiri upya matangazo ili waombe upya na kufanya usaili upya.


Aidha Sekretariet hiyo imebainisha kuwa zoezi ya uhakiki wa watumishi hewa bado linaendelea, na kwamba wakipewa ruhusa ya kutangaza ajira wakati wowote watatangaza.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts