Daktari Akwamisha Kesi Ya Scorpion | BONGOJAMII

Daktari Akwamisha Kesi Ya Scorpion

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Ushahidi katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili, Salum Njwete (34) maarufu Scorpion, umeshindwa kuendelea baada ya upande wa Jamhuri kudai shahidi hakufika.


Sababu za kutofika kwa shahidi huyo ambaye ni daktari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ni kutokana na kuwa nje ya kituo chake cha kazi hivyo hakupatikana jana.


Mshitakiwa Scorpion alipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule, wakati shauri hilo lilipopelekwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi upande wa Jamhuri.


Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai upande wa Jamhuri ulipanga kumhoji shahidi ambaye ni daktari lakini kwa vile alikuwa na dharura ingefaa mahakama impangie tarehe nyingine.


“Mheshimiwa hakimu shauri lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na upande wa Jamhuri ulipanga kumleta shahidi ambaye ni daktari lakini ameshindwa kufika leo, ana dharura ambayo inaweza ikachukua wiki tatu.


“Hivyo kwa mujibu wa kifungu namba 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi ya Makosa ya Jinai ambayo inataka kesi isiahirishwe zaidi ya wiki mbili kama mshitakiwa yuko mahabusu, tunaomba mahakama itaje hapa tupange tarehe ya kusikilizwa,’’alisema.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts