Hii sasa ni hatari, Mazombi Yavamia Ofisi za Cuf Znz,Yafanya Uharibifu Huu..! | BONGOJAMII

Hii sasa ni hatari, Mazombi Yavamia Ofisi za Cuf Znz,Yafanya Uharibifu Huu..!

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD



Ofisi ya Chama cha Wananchi (CUF) Jimbo la Dimani Wilaya ya Magharibi B imevamiwa na watu wasiojulikana maarufu mazombi.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali amesema tukio hilo lilimetokea saa 6.30 usiku wa kuamkia jana.


Amedai kuwa mazombi hayo yalipora mali, kujeruhi watu na kuwateka wengine wa nyumba jirani na ofisi hiyo.


“Ni kweli taarifa tunazo za watu kuvamia ofisi hiyo ya CUF na kuwapiga pamoja na kuwahujumu watu na huo ni uharamia unaoripotiwa mara kwa mara,” amesema Kamanda Ali.


Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa CUF, Salim Abdallah Bimani amesema, “Huu ni uvunjifu wa amani na tunataka Rais John Magufuli iwapo anayo nia ya dhati afuatilie hujuma hiyo ambayo watekelezaji wake wanajulikana lakini hawakamatwi.”
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts