Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
DAR ES SALAAM: Mwa n amu z i k i wa Taarab, Mariam Mohammed Uwesu ‘Mariam BSS’ Jumapili aliyopita alijikuta akimwagiwa kojo wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ‘bethidei’ iliyofanyika huko Manzese katika baa inayojulikana kama Bar Mpya, jirani na Friends Corner Hotel.
Katika hafla hiyo iliyosindikizwa na Kundi la Taarab la Diamond Classic Modern usiku huo, mshiriki huyo wa zamani wa shindano la kusaka vipaji la BSS, alimwagiwa pombe, maji machafu, soda na ndoo ya chooni iliyokuwa na mikojo wakati wa tukio la kufungua shampeni, ambalo kwa desturi mpya ya sasa, mhusika humwagiwa kinywaji hicho, sambamba na maji na vinywaji vingine laini.
Mambo yalienda vizuri hadi mshereheshaji katika tukio hilo, Mc Andamakopa alipotangaza kuwa wakati wa kufungua shampeni umefika na mara tu baada ya kinywaji hicho kufunguli wa, wageni wa alikwa walianza kummwagia kwa staili ya kumuogesha.
Kitendo hicho kiliamsha shamra kwa watu waliokuwepo, wakiwemo ‘masela’ ambao nao walimvamia na kuanza kummwagia vimiminika mbalimbali zikiwemo pombe kali, soda na maji machafu.
Wakati hayo yakiendelea, wanaosadikika kuwa masela, walienda chooni na kuchukua ndoo ya maji yaliyochanganyika na mikojo na kwenda kummwagia mwilini hali iliyosababisha baadhi ya wasamaria wema kumchomoa katikati ya kundi hilo baada ya kushtukia harufu kali ya mkojo.
Baada ya kuchomolewa alikimbizwa chooni kwenda kuoga ndipo mambo mengine yakaendelea huku mwanamuziki huyo akiwalalamikia waliomfanyia kitendo hicho akisema hakikuwa cha kiungwana.
“Ukweli suala la kumwagiana shampeni au maji ni la kawaida, lakini kitendo walichonifanyia cha kunimwagia maji machafu yanayonuka harufu ya mikojo si cha kiungwana.
“Ile ndoo wameitoa chooni na si unajua vyoo vya baa, walevi wengine wakienda kukojoa hawaangalii, wanakojolea hata maji ya kunawa , ” alilalamika Mariam.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka