Aibuuuu==> Mwalimu Afumaniwa na Mwanafunzi Wake Kitandani | BONGOJAMII

Aibuuuu==> Mwalimu Afumaniwa na Mwanafunzi Wake Kitandani

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agness Hokororo amemuweka rumande Mwalimu mmoja wa Shule ya Sekondani Matolo kwa madai ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo.

Hokororo alisema kuwa tukio lilitokea jana baada ya Mwalimu huyo kuwekewa mitego na wazazi wa mwanafunzi huyo. Ilidaiwa kuwa siku ya tukio , mwanafunzi huyo alitoroka nyumbani usiku na kwenda kulala na kwenda kulala nyumbani kwa Mwalimu huyo.

Alisema wazazi na baadhi ya majirani waliizingira nyumba ya Mwalimu huyo na kisha walimpigia simu ili akashuhudie tukio hilo. “Kwakweli ni jambo la kusikitisha. Nilifika katika nyumba ya Mwalimu asubuhi saa 12 na kukuta akiwa na mwanafunzi huyo ambaye alikiri kuwa amekuwa akitoroka mara kwa mara na kuja kulala kwa Mwalimu wake,” alisema Hokororo.

Mwanafunzi huyo amesema huwa analala huko, alfajiri huwa anawahi nyumbani kwa ajili ya kujiandaa kwenda shuleni. Mwalimu huyo pia anadaiwa kumpa mimba mwanafunzi aliyetakiwa kumaliza kidato cha nne mwaka jana.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts