Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alimtaja kama Elius Msigwa aliyekuwa akiwababaisha wananchi wa maeneo ya Kivule anakoishi, alifukuzwa kazi tangu Disemba mwaka jana.
Alisema wakati mtuhumiwa huyo anafukuzwa ndani ya jeshi hilo, alikuwa na cheo cha Koplo, lakini alipokamatwa alikuwa amevaa cheo cha Sajenti na alikiri kuwa alifanya hivyo kutokana na kukosa nauli ya daladala.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwa nia ya kuomba radhi, kijana huyo ambaye alikuwa akifanya kazi katika gereza la Keko, alisema “Bahati mbaya siku ya juzi sikuwa na nauli ya kwenda mjini ndio nikavaa hizi ‘uniform’ (sare). Nilikuwa nawaomba vijana wenzangu hata kama umeacha kazi, umefukuzwa au chochote, msivae ‘uniform’ na baada ya kutoka hapa nazirudisha hizi uniform katika kituo changu kilichokuwa cha kazi,” alisema Msingwa.
Kamishina Sirro pia alisema jeshi hilo lilikamata watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi katika maeneo ya Kivule, Ukonga wakijihusisha na wizi wa kutumia silaha aina ya mapanga, kuvuta bangi na kunywa gongo.
By: Emmy Mwaipopo
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka