Diva Adai Hawezi Kutoka na Mwanaume Ambaye Hajui Kuongea Kingereza | BONGOJAMII

Diva Adai Hawezi Kutoka na Mwanaume Ambaye Hajui Kuongea Kingereza

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva The Bosslady amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kudate na mwanaume ambaye hajui kuongea kingereza kwa kuwa yeye katika maisha yake huongea kingereza zaidi kuliko kiswahili.

Akiongea na waandishi wiki hii, Diva amedai wanaume ambao amewahi kutokana nao wanazungumza lugha hiyo ambayo amedai inamvutia sana.


“Sipendi mwanaume ambaye hajui kingereza, napenda kudate na mwanaume ambaye anajua kingereza,” alisema Diva. “Yaani imetulia na inapendeza kwa sababu siyo local local, wapo ambao waliwahi kunitokea lakini baada ya kujua hawajui kingereza nikawatosa,”
Alisema wanaume wake wengi anakutana nao kwa mara ya kwanza kupitia kipindi chake cha Ala za Roho kwa kuwa ndio sehemu ambayo atakutana na watu mbalimbali.

Mtangazaji huyo ambaye pia ni muimbaji wa muziki kwa sasa anatoka kimapenzi na muimbaji ‘Heri Muziki’.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts