Hatimaye==>>Serikali yawasafirisha waliofukuzwa Msumbiji | BONGOJAMII

Hatimaye==>>Serikali yawasafirisha waliofukuzwa Msumbiji

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mtwara. Baada ya Watanzania wanaoishi nchini Msumbiji kufanyiwa vitendo vya kikatili na kufukuzwa, Serikali mkoani hapa imelazimika kuwasafirisha kwa kutumia magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ili kuwafikisha karibu na mikoa wanakotokea.

Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama amesema hadi kufikia juzi, Watanzania waliojisajili katika mpaka wa Kilambo wakitokea Msumbiji walikuwa 220.

Amesema tayari watu 109 wa awamu ya kwanza wamesafirishwa, ambao waliishukuru Serikali na wakazi wa Mtwara kwa kuwapokea na kuwapa misaada mbalimbali.

Mmoja wa waliorudishwa, Mwajuma Abdallah amesema: “Tunawashukuru wanamtwara na Serikali kwa jumla kwa kutupokea vizuri leo (jana) tunarudi nyumbani.”
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts