Sakata la Madawa ya Kulevya Ridhiwani Afunguka==>>Sifanyi Biashara Hiyo Haramu Wala Sijawahi Kufikiria, Nafsi Iko Radhi Kufa Masikini | BONGOJAMII

Sakata la Madawa ya Kulevya Ridhiwani Afunguka==>>Sifanyi Biashara Hiyo Haramu Wala Sijawahi Kufikiria, Nafsi Iko Radhi Kufa Masikini

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amekanusha vikali shutuma zilizotolewa dhidi yake kuhusu kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya 

Moja ya magazeti ya jana yalichapisha habari inayomtaja mbunge huyo kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya ambayo imekuwa ikipigwa vita kila kona ya nchi kutokana na kupoteza nguvu kazi ya taifa 

Gazeti hilo limeandika kuwa jina la Ridhiwani limetajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya na kuwa uchunguzi utafanyika. Pia limesema mbunge huyo ametoa kauli nzito kwa hadhara 

Kiongozi huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa,'hafanyi biashara hiyo haramu wala hakuwahi kufikiria kuifanya na kwamba nafsi yake i tayari kufa masikini kuliko kupata utajiri kupitia njia hiyo 

Aidha, ameeleza kuwa anaamini kwamba uchunguzi utafanywa ili kuweza kuweka mambo sawa kwani yeye hana kitu chochote cha kuficha. Amesema kwamba, maneno hayo ya shutuma juu yake ni uongo na kwamba yametolewa na watu wasiomtakia mema na wasio na haya.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts