BALAA HILI, MUUGUZI ACHOMWA MOTO ADI KUFA KWA KUMPA HUDUMA MBOVU MGONJWA | BONGOJAMII

BALAA HILI, MUUGUZI ACHOMWA MOTO ADI KUFA KWA KUMPA HUDUMA MBOVU MGONJWA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Muuguzi mmoja nchini Israel amefariki baada ya kuchomwa akiwa hai na mgonjwa katika eneo la Holon kusini mwa Tel aviv.


Tova Kararo mwenye umri wa miaka 56 alimwagiwa mafuta na kuchomwa baada ya kujibizana na mgonjwa ambaye alikuwa hajaridhika kulingana na afisa mmoja wa polisi.


Mshukiwa huyo ambaye yuko katika umri wa miaka 70 alitoroka eneo la mkasa huo kwa kutumia gari lakini akakamatwa baadaye.


Vyombo vingi vya habari nchini Israel vimeripoti kwamba mshukiwa huyo alikuwa manusura wa holocaust anayeugua ugonjwa wa akili.


Mkuu wa polisi katika eneo hilo Sigal Bar Tzvi alisema kuwa mtu huyo aliwasili katika kituo hicho cha afya na alidaiwa kwamba hakuridhishwa na matibabu aliyopata.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts