HAPA NDIPO ILIPOFIKIA KESI YA MREMBO AGNES MASOGANGE | BONGOJAMII

HAPA NDIPO ILIPOFIKIA KESI YA MREMBO AGNES MASOGANGE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Upelelezi wa kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange(28) katika Mahakama ya Kisutu bado haujakamilika.


Wakili wa Serikali, Adolf Mkini ameeleza hayo leo wakati kesi ilipotajwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri.


Mkini alidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na mshtakiwa hayupo mahakamani hapo.


Baada ya kueleza hayo, wakili wa Masogange, Nictogen Itege ameiambia Mahakama kuwa mteja wako hiyo alikuwa njiani kuelekea mahakamani lakini alikwama katika foleni eneo la Jangwani.


Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts