SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA, DJ MAJIZZO AENDA TENA CENTRAL KUHOJIWA LEO | BONGOJAMII

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA, DJ MAJIZZO AENDA TENA CENTRAL KUHOJIWA LEO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Taarifa zilizotufikia, zinaeleza kwamba mmiliki wa EFM na Dj maarufu Bongo, DJ Majizo, mchana wa leo ameenda kuripoti tena kwenye Kituo Kikuu cha Polisi (Sentro) na kuhojiwa kwa mara nyingine kuhusu sakata lake la kuhusishwa na biashara ya madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Majizo alionekana Sentro majira ya mchana, leo Machi 14, 2017 ambapo baada ya kuhojiwa, aliachiwa na kuondoka zake.
Hii inakuja siku chache baada ya Majizo, kukamatwa na kushikiliwa kwa siku kadhaa kwenyekituo hicho cha polisi, baada ya kukamatwa, akihusishwa na biashara ya madawa. Majizo ni miongoni mwa mastaa kadhaa Bongo, ambao wamekumbwa na msukosuko, tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuanza kutaja majina ya watu wanaodaiwa kujihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya.
Wengine waliowahi kushikiliwa na baadaye kuachiwa kwa sakata hilo, ni Khaleed Mohamed ‘TID’, Tunda Sebastian, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, Winfrida Josephat ‘Rachel’, Hamid Salim ‘Nyandu Tozi’, Ceud Mandigo ’Babu wa Kitaa’, Wema Sepetu ‘Madam’ , George Romeo ‘Rommy Jones’, Ahmed Hashim ‘Petit Man’ na Vanessa Mdee ‘V-Money’.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts