SIRI NZITO YAFICHUKA==>> KUMBE KADA WA CHADEMA ALIYE UAWA NI SHAHIDI KESI YA MADAWA YA KULEVYA | BONGOJAMII

SIRI NZITO YAFICHUKA==>> KUMBE KADA WA CHADEMA ALIYE UAWA NI SHAHIDI KESI YA MADAWA YA KULEVYA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Moshi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amedai kuwa kada wa Chadema, Anitha Kimario (44) aliyeuawa alikuwa awe shahidi katika kesi moja dawa za kulevya.

Mutafungwa amesema kiini cha mauaji hayo kinachunguzwa.

Shauri hilo linamhusisha kinara wa usafirishaji wa bangi kwenda nchini Kenya, kupitia njia za panya zilizopo mpakani wilayani Rombo.

Kamanda Mutafungwa amesema polisi wanachunguza mazingira ya mauaji hayo ili kubaini waliohusika, huku akisema watu wawili wanashikiliwa kwa mahojiano.

Mutafungwa amesema juzi jioni polisi waliokota mwili wa mwanamke huyo ambaye pia ni mfanyabiashara ukiwa umetupwa kwenye mashamba ya miwa.

“Tulipofika eneo la tukio tulikuta mwili wake ukiwa umewekwa kwenye matuta ya kupandia miwa ukiwa umefunikwa na majani na udongo, umevuliwa nguo na kubaki na za ndani,” amesema.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts