HAYA NDIO MAMBO 7 YALIYOJITOKEZA KWENYE KIKAO CHA CUF NA KAMABDA SIRO | BONGOJAMII

HAYA NDIO MAMBO 7 YALIYOJITOKEZA KWENYE KIKAO CHA CUF NA KAMABDA SIRO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD


Amezungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF Julius Mtatiro


"Tumemaliza kikao na Kamishna Sirro (Mimi nikiambatana na Wakurugenzi wa kitaifa na Wajumbe wa Baraza Kuu wa CUF) ;


Kamishna Sirro ana roho ya kipekee sana ni Ofisa wa Polisi wa mfano, ametupokea na ametupatia ushirikiano mkubwa sana.


1. Tumempa barua rasmi na ushahidi wa matukio yote ya jinai ambayo chama kimetendewa tangu Agosti mwaka 2016 huku wafanya matukio hayo mabaya wakilindwa.


2. Tumezungumza kwa kina juu ya tukio la Uvamizi wa Vina Hotel na kutaka hatua zichukuliwe haraka.


3. Kamishna Sirro amesikitishwa sana kusikia kuwa viongozi wa chama wameitwa Magomeni ili wapatanishwe na wavamizi/majambazi/mungiki/mazombi. Sirro amekataa utaratibu huo na anasema kuwa makosa ya jinai hupelekwa mahakamani, hayasuluhishwi na Polisi.


4. Tumemkumbushia Kamishna matukio 13 ya jinai ambayo yametendwa na Lipumba na genge lake dhidi ya chama yakiwemo kuteka, kupiga, kuchoma visu, kuvamia n.k. tumemwambia kuwa katika matukio yote hayo, Lipumba na genge lake wameendelea kulindwa.


5. Tumemweleza Kamishna kuwa sisi tumeendelea kuwataka wanachama wawe watulivu ili tuone hatua za POLISI na kwamba hatua zisipochukuliwa, sisi tutachukua hatua.


6. Tumemkumbusha Kamishna Sirro kuwa sisi (chama) ni wengi kuliko Lipumba na Genge lake na kwamba wingi wetu ni silaha kubwa sana na kwamba tunao uwezo wa kuwasambaratisha mara 100 ikiwa tunataka. Lakini sisi bado ni wastahimilivu, tunataka kuona hatua zinachukuliwa na POLISI


7. Kamishna Sirro ameahidi kuwa anachukua hatua, ameelekeza mapungufu yetu, amekubali baadhi ya mapungufu yao na kutoa maelezo baadhi ya mambo muhimu. Hatuwezi kumhukumu Sirro kwa sasa, ila tutamhukumu tukishaona hakuna hatua zinazochukuliwa."

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts