HIKI NDICHO KINACHOENDELEA KUHUSU MKUTANO WA ROMA NA WAANDISHI WA HABARI | BONGOJAMII

HIKI NDICHO KINACHOENDELEA KUHUSU MKUTANO WA ROMA NA WAANDISHI WA HABARI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Dar es Salaam. Hali ya sintofahamu imeanza kujitokeza tokea leo asubuhi hadi saa 5: 48 baada ya mkutano aliotakiwa kuufanya Roma Mkatoliki na waandishi wa habari kushindwa kufanyika kwa wakati.

Mapema leo kaka yake Roma, Omary Musa amesema mkutano huo ungefanyika saa tano.

Hata hivyo Musa hakuweka wazi eneo la kufanyia mkutano huo kwa kile alichodai bado hawajapata eneo.

"Eneo tulilopata awali mwenyewe anaonekana kuwa na hofu, tunatafuta eneo lingine tutawajulisha kabla ya saa tano ila tunalenga maeneo ya Kinondoni, "amesema

Ilipofika saa tano mwandishi alimtafuta kujua eneo Musa akajibu bado hawajapata na huenda mkutano huo ungesogezwa hadi saa nane.

"Bado tunatafuta kuna watu wamepewa jukumu hilo, hatuwezi kufanyia popote lazima liwe eneo salama, hatujui waliomteka walikuwa na nia gani"


"Nipigie baada ya dakika 45 nitakuwa nimeshajua, muhimu kuweni na subira tutawataarifu," amesema

Jumamosi iliyopita baada ya kupatikana akiwa kituo cha polisi Osterbay Roma aliahidi kuzungumza na waandishi leo kuelezea kilichotokea

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts