INASIKITISHA: LORI LAUA WANAFUNZI 2 WAKITOKEA SHULE | BONGOJAMII

INASIKITISHA: LORI LAUA WANAFUNZI 2 WAKITOKEA SHULE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
WANAFUNZI wawili wa Shule ya Msingi Nyaruyoba Salima Hamza (10) na Nyamweru Matokeo (12), wakazi wa Kijiji cha Busunzu Wilaya ya Kibondo, mkoani Kigoma, wamefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na lori aina ya Scania na tela lake walipokuwa wanatoka shuleni.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Obadia Nselu, alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 9 alasiri katika kijiji hicho kwenye barabara ya Kibondo–Kasulu.

Nselu alisema gari hilo lilikuwa linaendeshwa na dereva Hatibu Mwalimu (39), mkazi wa Tanga.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni kukatika kwa kifaa ambacho ni kiungo cha tela la gari hilo na kusababisha tela kuacha njia na kuwagonga wanafunzi hao na kufariki dunia papo hapo.

Kaimu Kamanda huyo alisema marehemu Salma alikuwa anasoma darasa la kwanza na Nyamweru Matokeo alikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu.

Alisema dereva wa gari hilo alikamatwa na anashikiliwa na Jeshi la Polisi na uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea na baada ya kukamilika, dereva huyo atafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts