KIMENUKA, MWENYEKITI WA CHADEMA MKOANI TANGA AHAMIA CCM | BONGOJAMII

KIMENUKA, MWENYEKITI WA CHADEMA MKOANI TANGA AHAMIA CCM

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoani Tanga kimepata pigo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Muheza, Rwebangira Mathias Karuwasha kuamua kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) jana kutokana na chama hicho kupoteza dira na mwelekeo.


Lakini kubwa zaidi inatokana na mambo yanayofanywa na chama hicho kwa kuiondoa uhalisi wa chama hicho ambayo wananchi walikuwa wanaitegemea kuwa chama cha kuwa mshindani na CCM ili kuleta mabadiliko.


Hatua ya mwenyekiti huyo kutangaza kujiuzulu inakuja siku chache baada ya maamuzi wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama kanda ya kaskazini mjini Tanga uliokuwa chini ya Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe kuridhia kuvunja uongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya ya mkoa wa Tanga.


Akitangaza uamuzi huo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa BMK uliopo Sahare Jijini Tanga,Rwebangira Karuwasha alisema hayo ndio mambo makubwa yaliyopelekea kuamua kukaa pembeni na kujiunga na CCM ambako anaona kuna sera makini zinazotekelezeka .


Alisema kutokana na matukio mbalimbali anayoyafanya Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe sitegemei kuendelea kubaki kwenye chama hiki cha watumwa na watwana hivyo nimeamua kujiunga na CCM kwani ndio chama kinachoweza kutekeleza sera makini na zenye mafanikio.


“Kwa mfumo wa uongozi unaongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe haukubaliki na hakuweza kuvumilia…. sitegemei kuendele kuwepo kwenye chama hicho kilichokuwa cha watwana na watumwa hivyo nimeridhia kujiunga na CCM “Alisema.


“Kuanzia leo mimi sio mwanachama wa Chadema na nitajiunga na CCM ya sasa chini ya Rais Dokta John Magufuli sababu Chadema wameacha sera makini kwa ajili ya kuwapa maendeleo wananchi.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts