USAFIRISHAJI WA MKAA KUTOKA WILAYA MOJA HADI NYINGINE WAPIGWA MARUFUKU | BONGOJAMII

USAFIRISHAJI WA MKAA KUTOKA WILAYA MOJA HADI NYINGINE WAPIGWA MARUFUKU

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Dodoma. Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ametangaza mabadiliko katika biashara ya mkaa nchini na kusema kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu hakuna mkaa wowote utakaosafirishwa kutoka wilaya moja kwenda nyingine ili kunusuru misitu inayoteketea kwa kasi hapa nchini.

Amesema hayo leo wakati akifungua mkutano wa 24 wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma.

“Kuanzia mwezi Julai hakuna ruhusa ya kutoa vibali vya kuhamisha mkaa kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine, mkaa utachomwa, utauzwa ndani ya wilaya kwa ajili ya matumizi ya Watanzania wanaohitaji nishati ya mkaa, lakini biashara ya mkaa ya kutoa Dodoma kwenda Dar es Salaam mpaka Zanzibar marufuku.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts