VIDEO YA MAKONDA YAZUA TAFRANI KWENYE MKUTANO WA WAANDISHI NA ROMA | BONGOJAMII

VIDEO YA MAKONDA YAZUA TAFRANI KWENYE MKUTANO WA WAANDISHI NA ROMA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
HALI ya Taharuki imeibuka katika mkutano wa waandishi wa Habari na na Roma mara baada ya Waziri wa Habari Utamaduni, sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe asema kuwa kuonyeshwa Videos ya RC Makonda aliyopahidi kupatikana kwa Roma na wenzake kabla ya juma pili.
Taharuki hiyo imejitokeza leo kwenye mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo Roma Mkatoliki aliahidi kuongea na waandishi kuhusu kutekwa kwake.

Waziri Mwakyembe alifika kwenye ukumbi huo kwa ajili ya kuwatoa hofu watanzania pamoja na wasanii, wanamichezo na waandishi wa habari kuwa wasiwe na hofu.

Waandishi walitaka kujua uhusiano wa kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ya kudai kuwa anaimani kuwa Roma na wenzke watapatikana jumapili.

Waziri mwekyembe alipokuwa anajibu swali hilo Ofisa wa wa idara ya habari maelezo aliyekuwa akisimimia mkutano huo aliamuru maswali yasiendelee.

Makonda alinukuluiwa na baadhi ya vyombo vya habari vya kijamii akizungumzia suala la kutekwa kwa Roma siku ya Ijumaa ilhali Roma na wenzake walipatikana siku ya juma mosi.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts