MRISHO GAMBO ACHARUKA , ATOA ONYO KALI | BONGOJAMII

MRISHO GAMBO ACHARUKA , ATOA ONYO KALI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa tukio la msiba wa wanafunzi wa Lucky Vincent uliotokea hivi karibuni halikutegemewa na halipaswi kutumika kujinufaisha kisiasa

Aidha, Gambo alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Serikali imetwaa jukumu la kushughulikia suala hilo kutokana na ukubwa wake kwa taifa na kwamba, serikali haiko tayari kuona masuala ya msingi kwa taifa yakichanganywa na siasa.

“Naomba tuwaombee (majeruhi walioko hospitali)… na serikali tuliamua kubeba jukumu la msiba kwa sababu ni jambo zito, hivyo hatuko tayari kuona mambo ya msingi yanaingizwa siasa,” alisema.

Awali, akitoa taarifa ya vifo vya wanafunzi hao katika tukio la ufunguzi wa semina ya Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi za Jamii (TSSA) jijini Arusha, Gambo, amesema majeruhi Doreen Mshana, ameshafanyiwa operesheni tano na anaendelea vizuri pamoja na wenzake Saada Mshana na Wilson Tarimo. Majeruhi hao ni wanafunzi wa Lucky Vincent walionusurika katika ajali hiyo ya Mei 6 na kupelekwa Marekani kwa matibabu zaidi.



Alisema Arusha kwa sasa ni tulivu kwa sababu serikali yake iko makini katika kudhibiti watu wenye harakati za kuashiria ukosefu wa amani.
Aliongeza kuwa hivi sasa, wakihisi kuna mkusanyiko au maandamano yasiyo na tija huwa wanawahi kuwadhibiti wahusika kabla ya kuathiri wengine.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts