MVUA YASABABISHA MAPOROMOKO YA MAWE MKOANI TANGA, | BONGOJAMII

MVUA YASABABISHA MAPOROMOKO YA MAWE MKOANI TANGA,

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Jeshi la Polisi mkoani Tanga imefunga barabara ya kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha kufuatia eneo la Mombo mkoani Tanga kuangukiwa na maporomoko ya mawe pamoja na matope na kusababisha athari kwa baadhi ya magari

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani humo Benedict Wakuyamba amesema, maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo na maeneo mbalimbali nchini


"Hali ya mvua imeendelea kunyesha na kufukia barabara eneo la Mombo kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha ambapo matope na miti vimesombwa na kukwama barabarani hali iliyokwamisha magari makubwa kwa madogo kusafiri kupitia eneo hilo..Niwaombe abiria au wananchi kwa ujumla kama hawana ulazima wa kusafiri kwenda mikoa ya Kaskazini ni vizuri wakatulia kwa siku mbili tuone hali inakwendaje kwa ajili ya usalama wao". Alisema Kamishna Msaidizi Benedict
Kwa upande mwingine Kamishna huyo amesema TANROADS na Jeshi la Polisi mkoani humo wanaendelea kusaidia kuondoa magogo na tope zilizosakama katika barabara ili kunusuru hali ya usafiri

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts