SERIKALI KUSAFIRISHA MWILI WA MZEE NGOSHA | BONGOJAMII

SERIKALI KUSAFIRISHA MWILI WA MZEE NGOSHA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu alimaarufu kwa jina la Mzee Ngosha ambaye anayetajwa kuwa ni moja wa wachoraji wa nembo ya Taifa aliyefariki tarehe 30 mwezi wa 5 unatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea Misungwi Mwanza.


Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Maendeleo ya Jamii) imesema kuwa ndugu wa Mzee Kanyasu wamepatikana na sasa serikali itagharamia kusafirisha mwili wa mzee huyo mpaka Mwanza ambapo atakwenda kuzikwa huko.


Mwili wa Mzee Francis Maige unatarajiwa kuagwa leo Jumamosi saa 2 asubuhi Hospitali Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanza safari ya kuelekea Mwanza.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts