HARMORAPA AMLILIA MPENZI WAKE ALIEMKIMBIA | BONGOJAMII

HARMORAPA AMLILIA MPENZI WAKE ALIEMKIMBIA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msanii wa muziki wa bongo fleva Harmorapa, ameweka wazi kuwa amekimbiwa na aliyekuwa mpenzi wake, baada yakuingia kwenye muziki na kutoboa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Harmorapa amesema mpenzi wake huyo ambaye hajamtaja jina lake, alimuacha baada ya yeye kupata umaarufu, akihofia ataanza kumsaliti.

“Unajua mawasiliano yalikuwa yamepungua, na hakuna alichokifanya kunkosea au nilimkosea, unajua mapenzi haya alidai kwamba nishakuwa maarufu nitamuumiza, ila angevumilia tu”, alisema Harmorapa.

Harmorapa amesema kwa sasa hayuko kwenye mahusiano yoyote, tangu mpenzi wake huyo afunge vilivyo vyake na kuondoka zake.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts