MAAMUZI KESI YA WEMA SEPETU KUTOLEWA AUGUST 18 | BONGOJAMII

MAAMUZI KESI YA WEMA SEPETU KUTOLEWA AUGUST 18

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Agosti 18, 2017 itatoa uamuzi kuhusiana na kielelezo cha msokoto mmoja wa bangi na vipisi viwili vya bangi vipokelewe kama kielelezo ama la.


Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba katika kesi inayomkabili Mlimbwende wa Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu na wenzake wawili.


Ni baada ya Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kumuongoza ushahidi wa kwanza wa upande wa mashtaka, Mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima kuendelea kutoa ushahidi wake.


Ambapo alidai kuwa alipima msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kukutwa nyumbani kwa Wema na kugundua ni bangi.


Hata hivyo, Mulima kupitia Kakula aliomba kuitoa bahasha iliyofungwa juu yenye muhuri, saini ya shahidi huyo na namba ya maabara 291 ya 2017 mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.


Kakula alimuuliza ushahidi huyo baada ya Mahakama kuipokea bahasha hiyo, anakumbuka kuna vitu gani ndani ya bahasha hiyo?


Mulima alidai ndani ya bahasha kulikuwa na msokoto mmoja, vipisi viwili ndani yake vina majani ya bangi na akaomba shahidi huyo aifungue bahasha hiyo.


Shahidi aliifungua bahasha hiyo na kuomba kutoa msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi mahakamani kama kielelezo cha ushahidi.


Wakili Tundu Lissu alipinga kisipokelewe kama kielelezo cha ushahidi kwa sababu ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.


Alidai Lissu vipisi viwili vyenye majani ukiviangalia kwa makini ni vipisi vya sigara za kienyeji ambayo imetumika kwa sababu vina alama ya kuungua ambavyo kwao vinaitwa twagooso.


Lissu alibainisha kuwa kitu kinachoitwa msokoto wa bangi hakijulikani.


“Haiwezekani vitu vilivyotolewa kwenye bahasha kuwa ndiyo vitu shahidi alivielezea, mahakama isikubali kuvipokea kama kielelezo,” alieleza Lissu.


Kwa upande wa Wakili Kakula alidai kuwa amesikia mapingamizi ya upande wa utetezi na kwamba hayana msingi wowote kisheria.


Alidai kuwa wakati Shahidi wake anatoa ushahidi alieleza vitu vilivyokuwamo ndani ya bahasha msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi, hakuna kitu ambacho shahidi huyo kakisema kimekutwa hakipo.


Alibainisha kuwa huwezi kuongelea kila kitu bali vitu vya msingi na akaomba mahakama kupokea msokoto mmoja na vipisi viwili vya bangi kama kielelezo.


Lissu alisisitiza kuwa kila kilichomo kwenye bahasha hiyo iliyofungwa kilipaswa kutajwa na kwamba wateja wao wanakabiliwa na shtaka ambalo wakibainika wanahatia watafungwa.


Kutokana na hoja hizo Hakimu Simba alisema Agosti 18, 2017 atatoa uamuzi juu ya hoja hizo na kesi hiyo pia inaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.


Awali katika ushahidi wa Mkemia huyo, Mulima alidai kuwa Februari 8, 2017 akipokea sampuli ya mkojo wa Wema.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts