MUBENGA AINGILIA KATI BIFU LA OMMY DIMPOZ NA DIAMOND | BONGOJAMII

MUBENGA AINGILIA KATI BIFU LA OMMY DIMPOZ NA DIAMOND

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Stori kubwa kwa sasa ambayo imekuwa gumzo kwenye mitandano ni kuhusiana na ishu inayodaiwa kuwa ni beef kati ya mastaa wa Bongofleva, Diamond Platnumz na Alikiba ambapo kumekuwa na majibizano huku Diamond akitumia baadhi ya maneno yanayodaiwa kuwa ni vijembe.

Miongoni mwa walioguswa na vijembe hivyo ni Ommy Dimpozi ambaye baada ya kuguswa naye alirudisha kupitia Instagram yake.

Baada ya post yake Instagram Meneja wa zamani wa Ommy Dimpoz, Mubenga amemuandikia ujumbe kwa Ommy Dimpozi akiandika.

“Omary mdogo wangu maandiko yanasema waheshimu wazazi upate heri na Miaka mingi duniani na mzazi sio mpaka akuzae ata mzazi wa mwenzio pia ni mzazi wako why unamuingiza mama naseb kwenye mambo yenu? Uko ni kukosa adabu wew si unajifanyaga innocent kwa watu kumbe una pretend? Wew sindio uliyeimba nani kama mama imekuwaje leo una watusi wa kina mama?

“Au ndio stress za Mziki? Watu wanataka video ya cheche na sio kutusi wazazi wa watu usituaribie muziki wetu kama game imekushinda please kaa pembeni pia naomba vyama vyenye dhamana ya muziki vichukue atua kali zidi ya matusi ya omary kwa mama wa diamond ili iwe fundisho kwa wengine ya kwangu ni hayo tu! #supportedbybangerzent #Mazoea link kwenye bio yangu #TUWAHESHIMUWAZAZIWETU” – Mubenga

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts