Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mtandao wa habari nchini Afrika Kusini wa Eyewitness News, unasema kuwa Rais Robert Mugabe amebadilisha mipango yake ya safari kuweza kushughulikia suala linalomhusu mkewe nchini Afrika Kusini.
Msichana wa umri wa miaka 20 amemlaumu mke wake Mugabe, Grace kwa kumpiga kwa kifaa cha umeme wakati wa mzozo kwenye hoteli moja Jumapili jioni.
Bi Mugabe hakufika katika kituo cha polisi mjini Johannesburg baada ya kusema kuwa angefanya hivyo na hadi sasa hajazungumza lolote kuhusu madai hayo.
Kinyume na ripoti za awali kuwa Bi Mugabe alikuwa amerejea nchini Zimbabwe, mtandao wa Eyewitness pia unasema kuwa Bi Mugabe yuko bado nchini Afrika Kusini.
Rais Mugabe anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa 37 wa maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) mjini Pretoria wiki hii.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka