Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
WAKATI Yanga inawasili Songea juzi Alhamisi, jezi ya kiungo Papy Kabamba Tshishimbi ndiyo iliyokuwa ikiuzwa kwa wingi, lakini jana Ijumaa jezi ya straika Obrey Chirwa nayo iliuzwa kwa wingi.
Chirwa amekuwa nje ya uwanja kwa muda akiuguza majeraha ya misuli ya mguu wake, lakini sasa yupo vizuri na anaweza kucheza mechi ya leo dhidi ya Majimaji.
Yanga leo inacheza na Majimaji mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Majimaji ikiwa imetoka kuifunga Njombe Mji bao 1-0 wikiendi iliyopita.
Katika mitaa mbalimbali ya Songea, wafanyabiashara ndogondogo wanaonekana wakiwa na jezi zinazotumiwa na Yanga zenye jina na namba ya Tshishimbi na zile za Chirwa na wachezaji wengine wakiziuza kwa mashabiki.
Jezi hizo zinazouzwa nje ya utaratibu wa klabu, huuzwa kwa kati ya Sh 7000 hadi Sh 25,000 na mashabiki wamekuwa wakizichangamkia kuzinunua.
Juzi jezi ya Tshishimbi ilikuwa ikinunuliwa kwa wingi lakini jana Ijumaa ile ya Chirwa raia wa Zambia nayo ilinunuliwa kwa wingi.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka