MBUNGE CHADEMA KUPELEKA HOJA BUNGENI ,MUDA WA URAIS UPUNGUZWE | BONGOJAMII

MBUNGE CHADEMA KUPELEKA HOJA BUNGENI ,MUDA WA URAIS UPUNGUZWE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mbunge wa Tarime Vijijini kupitia (CHADEMA) John Heche amefunguka na kusema anakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi ili kupunguza muda wa viongozi kukaa madarakani kutoka miaka mitano na iwe miaka minnee kama Marekani.



John Heche amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii zikiwa zimepita siku kadhaa toka Mbunge wa Chemba Mhe. Juma Nkamia (CCM) kusema anatarajiwa kuwasilisha muswada binafsi bungeni kulitaka bunge kufanya marekebisho ya katiba ili viongozi waweze kukaa miaka saba. Jambo ambalo Heche anapinga na kusema kuwa muda ambao viongozi wanakaa madarakani ni mkubwa sana.


"Nakusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi kupunguza muda wa kukaa madarakani kwa Rais, wabunge na madiwani kutoka miaka 5 mpaka 4 tuwe kama Marekani ili kutoa nafasi kwa wananchi kuwa na maamuzi zaidi kuhusu uendeshaji wa nchi yao" Alisema John Heche


Aidha John Heche amesema kuwa kiongozi akikaa madarakani muda mrefu anajisahau na kuona ile nafasi kama ni yake pekee yake jambo ambalo si sawa hata kidogo


"ukikaa sana madarakani unafikiri nchi ni mali yako, kuna viongozi wengi sana wazuri ila hawajapata muda tu wa kuongoza" alisisitiza John Heche.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts