MLIPUKO WA BOMU WAUA WATOTO 3 JIJINI ARUSHA | BONGOJAMII

MLIPUKO WA BOMU WAUA WATOTO 3 JIJINI ARUSHA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Watoto watatu waliokuwa wakichunga ng'ombe wamefariki dunia baada ya kulipukiwa na bomu walilolichezea wakidhani ni mpira.


Tukio hilo lilitokea Ijumaa jioni katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale wilayani Monduli mkoa Arusha.


Mwenyekiti wa kijiji hicho, Julius Mhale amesema watoto hao wanatarajiwa kuzikwa kesho Jumatatu.


Amesema eneo lilikolipuka bomu hutumiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa mazoezi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa rasmi.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts