WASANII NA WATU MAARUFU WAUNGANA KULAANI TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI | BONGOJAMII

WASANII NA WATU MAARUFU WAUNGANA KULAANI TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Jana nchi ilizizima baada ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi zinazoelezwa kuwa 32 mjini Dodoma.

Mazungumzo katika mitandao yalichukuliwa na tukio hilo kila mmoja akiomwombea mbunge huyo baada ya risasi tano kuingia katika maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Watu maarufu hawakubaki nyuma kuelezea hisia zao kwa tukio hilo na hivi ndivyo baadhi yao walivyoandika katika mtandao wa Instagram wakiambatanisha na picha yake.

Shilole: Hatma ya maisha mtu yeyote anayo Mungu na si mwanadamu. Mungu mwenye kutoa uhai na uzima akupe nafuu mkuu. Watanzania tumeguswa na naamini una maombi ya wengi sana.

Aunty Ezekiel: Dah!Nakosa la kuongea mwenyezi Mungu tenda miujiza yako.

JB: Naamini Mungu atakuponya na utarudi katika afya yako...Tunakuombea..Mungu atafanya.

Diamond: InshaAllah mwenyezi Mungu akusmamie na kukurudishia afya njema

Irene Uwoya: May you get a quick recovery honourable in God's power....My prayers are with you!!Amen

Idris: At This point tupunguze uchama kuhakikisha Tundu Lissu anakuwa stable, baada ya hapo tutajua nchi imekuwa ya namna gani.

Benpol: Pray for Tundu Lissu
Roma: God. Amen
Jux: #Prayfortundulissu

Lulu: Tuweke pembeni tofauti ya vyama na maono ya kisiasa...kwa sasa kwa imani/dini zetu tumuombee kama mtoto wa mama na baba fulani, mume wa mama fulani, baba mwenye watoto, familia na watu mbalimbali wanaotemgemea. Tusimuombee Tundu Lissu mbunge au mwanasiasa, tumuombee Tundu Lissu wa kawaida kabisa kama baba yetu, kaka yetu au mtu yeyote wa kawaida tunayemjua.

Lady Jay Dee: Mwenyezi Mungu aliyekuumba akakuinue kutoka kwenye kitanda walichokulaza binadamu tusiowafamu. Huwa tunaamini kwa jina la baba, la mwana na la roho mtakatifu.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts