Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewaambia waandishi wa habari pamoja na baadhi ya madaktari kutoka hospitali za serikali na za Binafsi kwamba taratibu zote za zoezi hilo zimekamilika hivyo amewahamasisha imiza wananchi kujitokeza katika zoezi hilo ambalo litakuwa na madaktari bingwa.
Baadhi ya Magonjwa yatakayohusika katika upimaji huo ni pamoja na Tezi Dume, kansa ya titi na shingo ya uzazi, shinikizo la damu pamoja na magonjwa yote yasiyopewa kipaumbele ambayo yamekuwa yakisababisha athari kubwa kwa binadamu. Aidha Bwana Makonda ameelekeza kutolewa tiba bure kwa wale watakaobainika kusumbuliwa na magonjwa.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka