BREAKING NEWS==>>AJALI MBAYA YA LORI LA MBAO YAUA NA KUJERUHI WATU 32 IRINGA | BONGOJAMII

BREAKING NEWS==>>AJALI MBAYA YA LORI LA MBAO YAUA NA KUJERUHI WATU 32 IRINGA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD



Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 32 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Vitu Laini linalofanya safari zake kutoka vijiji vya Kilolo kwenda Iringa Mjini kugongana na lori la mbao karibu likiwa limekaribia kufika Iringa Mjini.
Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Peter Kakamba amethibitisha kutokea kwa ajli hiyo na kueleza kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.“Ni kweli ajali imetokea leo asubuhi nje kigogo ya Mji wa Iringa, basi ndilo limelogonga lori kwa nyuma na kusababisha kifo cha mtu mmoja aliyeaga dunia palepale na kusababisha majeruhi 32.
“Majeruhi wote tumewapeleka katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa ambako wanaendelea kupatiwa matibabu mpaka sasa.Alisema Kamanda Kakamba.Kuhusu chanzo cha ajali hiyo haijafahamika kama ni matatizo ya gari au mwendoksasi wa dereva hivyo Kamanda Kakamba amesema watatoa taarifa rasmi baabdaye kuhusu tukio hilo.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts