HATIMAYE BOMOA BOMOA YAANZA BUGURUNI DAR ES SALAAM | BONGOJAMII

HATIMAYE BOMOA BOMOA YAANZA BUGURUNI DAR ES SALAAM

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Wakazi wa Buguruni wakiangalia tukio la ubomoaji wa nyumba zilizo ndani hifadhi ya reli.
Dar es Salaam. Nyumba zaidi ya 250 zilizopo pembezoni mwa reli ya kati, kuanzia Stesheni hadi Pugu zimeanza kuvunjwa leo (Jumamosi) na Kampuni hodhi ya rasilimali za reli nchini (Rahco) kwa kile kinachodaiwa kuwa zipo ndani ya hifadhi ya reli.

Wakati nyumba za Buguruni zikivunjwa leo wakazi wa eneo hilo wameilalamikia Serikali kwa kutotoa taarifa mapema jambo ambalo limesababisha baadhi yao kushindwa kuokoa mali walizonazao huku wengine wakiwa njia panda kwa kutofahamu ni wapi watalala.

"Suala la kuvunja sisi hatulikatai kama linakuwa limefuata sheria, tatizo uvunjaji wa leo ulikuwa na notisi ya siku moja, taarifa tulipewa jana leo wanakuja kuvunja. Awali tulijua hifadhi ya reli kwa eno la mjini ni mita 15 leo wanasema ni mita 30," amesema Elizabeth Mai, ambaye nyumba yake imevunjwa.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts