KIMENUKAA, SHILOLE AMTOLEA POVU KHADIJA KOPA | BONGOJAMII

KIMENUKAA, SHILOLE AMTOLEA POVU KHADIJA KOPA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msanii Shilole ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Sitoi kiki' amefunguka na kuwataja wasanii watano wa bongo fleva ambao yeye anawakubali na kupenda kazi zao.


Shilole alifunguka hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema katika wasanii hao msanii wa kwanza kabisa anayemkubali ni Bi. Khadja Kopa 


"Jamanii mimi nampenda sana huyu mama Khadja Kopa, nampenda sana sana lakini mbali na huyo pia napenda kazi za msanii Linah Sanga, Mwasiti, Diamond Platnumz pamoja na huyo kijana huyu ambaye ameniimba, anaitwaa RayVanny" alisema Shilole 


Mbali na hilo Shilole anasema hakubatika kwenda kwenye harusi ya Nuh Mziwanda sababu alikuwa na mishe zake zingine lakini amedai siku ya arobaini ya mtoto wake atakwenda kumuona mtoto na kumpa pongezi kwa kubarikiwa kupata mtoto.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts