MOSE IYOBO AFUNGUKA, ASEMA HATOACHA KUNENGUA NG'OO | BONGOJAMII

MOSE IYOBO AFUNGUKA, ASEMA HATOACHA KUNENGUA NG'OO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
MNENGUAJI wa kundi la Wasafi Classic (WCB), Moses Iyobo, amesema hajawahi kufikiria kuwa mwimbaji kwakuwa ni kazi inayohitaji kutumia akili nyingi tofauti na unenguaji.


Iyobo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina yake ya uchezaji, amesema ataendelea kubaki kuwa mnenguaji katika maisha yake yote sambamba na kuwa mwalimu kwa wenzake.


Alisema kazi ya kuimba inahitaji akili nyingi ili kufikia malengo hivyo ataendelea kubaki na kazi yake ya unenguaji.


“Nitabaki kuwa dansa maisha yangu yote, labda nitakachoongeza hapo ni kuwa mwalimu na kuwafundisha wengine, unajua kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe. Sasa kwa upande wangu sitaweza ni bora nibaki huku huku ndio pananifaa zaidi,” alisema Iyobo ambaye ni mpenzi wa msanii Aunt Ezekiel.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts