RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKAMISHNA SITA WA JESHI LA UHAMIAJI | BONGOJAMII

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MAKAMISHNA SITA WA JESHI LA UHAMIAJI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Rais John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa sita wa Uhamiaji kuwa Makamishna kuanzia februari 28, mwaka 2017 na kuwateua kushika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi hilo.


Wateule hao ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Peter Chogero kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala pamoja na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Samwel Rhobby Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi wa Mipaka.


Wengine ni Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald John Kihinga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Musanga Mbusuro Etimba ambaye anakuwa Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi.


Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Hennerole Morgan Manyanga ameteuliwa kuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria.


Rais amemteua pia naibu Kamishna wa Uhamiaji Mourice David Kitinusa kuwa Kamishna Chuo cha Uhamiaji cha kikanda (TRITA)


Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projest Rwegasira, amesema kuwa uteuzi huo unaanzia februari 28, mwaka 2017.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts