VIDEO==>> MANENO YA RAIS MAGUFULI KUHUSU WATU WENYE VYETI FEKI... | BONGOJAMII

VIDEO==>> MANENO YA RAIS MAGUFULI KUHUSU WATU WENYE VYETI FEKI...

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
DAR ES SALAAM: Siku za hivi karibuni kumekuwa na mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu suala la elimu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Watu wengi wamedai kuwa Makonda ametumia cheti cha mtu mwingine kidato cha nne baada ya yeye kuwa amefeli hivyo asingeweza kupata nafasi ya kujiunga na kidato cha tano na cha sita.

Kiongozi huyo hajazungumza lolote kuhusu tuhuma hizi zinazoendelea maeneo mbalimbali ya jamii.

Tukijikumbusha nyuma kidogo wakati Rais Dkt Magufuli alipofanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam mwaka, alizungumzia suala la watu kughushi vyeti na wengine kusema wana viwango vya elimu ambavyo kiuhalisia hawa.

Kuna watu wako hapa wanasema wa masters (shahada ya umahiri) na wengine wanasema wana PhD (shahada ya uzamivu), kwani nani amekwambia kufanya kazi lazima uwena ‘mastaers au PhD? alihoji Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema lengo la serikali kuhakiki vyeti vya watumishi haikuwa kuwafukuza kazi, lakini kuhakikisha kuwa kila anayelipwa fedha, analipwa kutokana na kiwwango chake cha elimu.

Hapa chini ni kauli aliyoitoa Rais Magufuli Septemba 26, 2016 alipofanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam kuhusu uhakiki wa vyeti vya watumishi wa serikali.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts