BAADA YA KUNUSURIKA KWENDA SELO, SASA NAY WA MITEGO KUACHIA VIDEO YA WIMBO "WAPO" MUDA WOWOTE | BONGOJAMII

BAADA YA KUNUSURIKA KWENDA SELO, SASA NAY WA MITEGO KUACHIA VIDEO YA WIMBO "WAPO" MUDA WOWOTE

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Msanii wa muziki wa hip hop, Nay wa Mitego amewataka mashabiki wake wa muziki kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa video yake mpya ya wimbo ‘Wapo’ ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Rapa huyo aliiambia Bongo5 kuwa kabla ya kufanya remix ya wimbo wake huo kama alivyoagizwa na Rais Magufuli, ataachia kwanza video ya wimbo huo.

“Nakukabidhi sindano ya kulidunga, daktari haogopi ukubwa wa kidonda, we si doctor wa majipuu tumbua hakuna kuvunga.. #Wapo Video kesho iko tayari. Subscribe kwenye YouTube Channel yangu sasa #MrNay,” Nay wa Mitego aliandika Instagram.

Awali wimbo huo ulifungiwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa kigezo cha maadili na baadae Rais Magufuli kutaka wimbo huyo upigwe kwa madai hauna tatizo kama baadhi ya taasisi nyingine za serikali zilivyodai.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts