CAG AONYA WATUMISHI WA SERIKALI KUKAIMU KWA MUDA MREFU | BONGOJAMII

CAG AONYA WATUMISHI WA SERIKALI KUKAIMU KWA MUDA MREFU

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Watumishi 422 wa Serikali na mamlaka ya serikali za mitaa wanafanya kazi kinyume cha sheria kwa kukaimu vyeo kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita, inaeleza ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akisoma ripoti hiyo ya mwaka 2015/16 mbele ya waandishi wa habari wiki iliyopita mjini Dodoma, CAG, Profesa Mussa Assad alisema kati ya hao watumishi 49 ni wa taasisi 14 za Serikali, na wengine 373 katika idara au vitengo vya mamlaka 78 za serikali za mitaa.

Profesa Assad alisema hali hiyo inakiuka agizo la Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009 zinazozuia mtumishi kukaimu nafasi ya wazi kwa muda unaozidi miezi sita.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa jambo hilo linatokana na Serikali kuanzisha mamlaka mpya za serikali za mitaa bila ya kuwa na mpango thabiti wa ujazaji nafasi za utumishi.

“Kushindwa kuwathibitisha maofisa katika nafasi wanazokaimu, kunaongeza madeni yatokanayo na posho za kukaimu,” inasema ripoti hiyo.

Professa Assad ameshauri mamlaka za serikali za mitaa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kupunguza idadi ya maofisa wanaokaimu kwa kuwathibitisha au kufanya uteuzi wa maofisa wapya wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi hizo.

“Kukaimu kwa muda mrefu kunapunguza ari ya utendaji kazi kwa maofisa wanaokaimu katika kufanya vizuri katika nafasi zao na kutoa huduma kwa ufanisi,” inasema ripoti hiyo.

Mamlaka zilizotajwa kuwa na idadi kubwa ya maofisa wanaokaimu nafasi za ukuu wa idara na vitengo ni halmashauri za wilaya ya Itigi, Msalala na Chemba.

Maoni ya wasomi
Akizungumzia suala hilo, wakili wa kujitegemea Profesa Abdallah Safari alisema mambo kama hayo yanatokea kutokana na uzembe wa watu kwa sababu sheria na taratibu zinakuwa zipo wazi lakini watu wanaamua kuzipuuza.

“Ukitaka kujua kuwa mfumo wa nchi haueleweki, angalia jinsi ambavyo Tanzania tumeandika historia ya nafasi ya Jaji Mkuu kukaimiwa wakati kwa nafasi kama yake kiongozi anayepaswa kumteua anakuwa na taarifa za anayestaafu miezi mitatu kabla,” alisema.

Profesa Safari, ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Chadema, alisema hawezi kushangaa jambo hilo likiwa hadi katika ngazi ya halmashauri.

Akizungumzia hilo, Profesa George Shumbusho, ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, alisema bora CAG amemulika suala hilo kwa sababu linaathiri utendaji wa kiongozi anayekaimu nafasi hiyo kwa kuwa anashindwa kupanga na kufanya vitu vingi vizuri kwa maendeleo ya ofisi yake.

“Mtu anapokaimu kwa muda mrefu anashindwa kufanya kwa ufanisi baadhi ya maamuzi, kama kumchukulia mtu hatua za kinidhamu na kuweka mikakati ya kimaendeleo kwa sababu anakuwa na hofu ya kutokamilisha kitu anachokipanga,” alisema.

Shumbusho alisema kiongozi anapokaimu kwa muda mrefu anashindwa kufanya baadhi ya maamuzi kwa kuwa muda wowote nafasi hiyo inaweza kujazwa na mtu mwingine.

Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema suala hilo linatokana na mfumo wa kiutawala unavyoendesha mambo yake, huku Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa imefanya mabadiliko mengi.

“Jambo lililofanyika ni ukiukwaji wa sheria na linaweza kuwa na athari kwa kusababisha mkanganyiko wa kiutawala”.

Alishauri kuwa iwapo viongozi wakiachwa kukaimu kwa muda mrefu, Serikali inaweza ikajikuta inaingia gharama kulipa watu wawili katika nafasi moja.

Suala kama hilo lilijitokeza katika ripoti ya CAG ya mwaka 2014/15 ambayo pia ilionyesha kuwa posho za watumishi wanaokaimu nafasi, hazikatwi kodi na hivyo kushauri wahusika wahakikishe makato hayo yanafanyika. 

Featured Posts