Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
KAMPUNI ya Simon Group, iko katika hatua ya mwisho ya mazungumzo na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), kwa ajili ya kupata eneo la kujenga kiwanda cha kuunganisha magari nchini, ikiwemo mabasi ya mradi wa mwendokasi wa jijini Dar es Salaam, na kuzalisha matairi.
Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum jana, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha Simon Group, Deus Buganywa alisema kampuni hiyo imeomba kwa NDC kupatiwa ekari 100 wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa ajili ya kutekeleza uwekezaji huo.
“Duniani kote hakuna anayetengeneza magari bali huchukua vifaa kutoka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuyaunga," alisema Buganywa. "Nasi tutakachofanya ni kuunga mabasi na malori nchini.”
Buganywa alisema upo uwezekano wa mabasi ya Udart kutoka nchini China yanayotumika sasa kwenye mradi wa mwendokasi (BRT) jijini Dar es Salaam, yakaja kuungwa nchini chini ya mradi huo.
Kwa mujibu wa Buganywa, kiwanda cha matairi kitajengwa katika eneo hilo la Kibaha pia kwa ajili ya kutengeneza matairi ya aina mbalimbali ambayo yana soko nchini.
“Tumelenga soko la magari ya serikali (kwa sababu) hilo ni soko la uhakika zaidi," alisema Buganywa.
"Kwa kuanzia tutaagiza malighafi kutoka nje wakati tunasubiri mashamba yetu ya Kalunga mkoani Morogoro na Kihuhwi mkoani Tanga kuzalisha mpira wa kutosha.”
Mashamba ya Kalunga na Kihuhwi katika eneo la ukubwa hekta 510 yako chini ya NDC, na kwa sasa yana mpira uliopandwa miaka ya 1970 ambao umezeeka.
Eneo jingine la ukubwa wa zaidi ya hekta 900 lina mpira mdogo ambao uvunaji wake unatarajiwa kufanyika baada ya miaka saba.
Alisema kwa sasa hakuna kiwanda cha matairi nchini na hivyo kulazimika kuagiza kutoka nje, na kwamba wanatumia mwanya huo kuzalisha kwa kutumia malighafi ya nje.
“Tunatarajia kuagiza teknolojia kutoka nje ya nchi. Kwa sasa tuko kwneye hatua ya mwisho ya mazungumzo na kampuni ya Advance Tire ya nchini China, ili tuendeshe kwa ubia kiwanda hicho.”
Alisema baada ya kukamilisha kiwanda cha uunganishaji mabasi "tutahamia kwenye malori".
ENEO LA VIWANDA
Mwishoni mwa mwaka jana Mkurugenzi wa NDC, Mlingi Mkucha aliieleza Nipashe kuwa wanatafuta wawekezaji kwa ajili ya eneo la viwanda lililotengwa mkoani Pwani, na kiwanda kimojawapo ni cha kuunganisha magari.
Kwa wakati huo alisema wapo kwenye mazingumzo na kampuni ya Tata ya India ili iweze kuwekeza kwa kuunga magari yake hapa nchini.
Mkucha hakupatikana kuzunguma majadiliano na Simon Group jana, hata hivyo.
Kiwanda cha matairi pekee kilichokuwepo nchini cha General Tyre kilifngwa mwaka 2009 kutokana na sababu mbalimbali, ikiwamo hujuma.
Kiwanda cha Sameer Investment cha nchini Kenya kilichoaanza baada ya General Tyre kufungwa, nacho kilifungwa Septemba mwaka jana sababu kubwa ikiwa ni kushindwa kuhimili ushindani wa matairi kutoka nje na kuongezeka kwa gharama za umeme.
Kiwanda cha General Tyre kipo mikononi mwa seriali kwa asilimia 100.
Katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka huu na hotuba ya bajeti ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka 2016-17, serikali imedhamiria kufufua kiwanda hicho na ilishatoa Sh. milioni 150 kwa ajili ya kupanda mpira kwenye mashamba ya mpira.