Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Wachezaji wa timu ya Mbao FC
KIPA wa Mbao, Erick Ngwengwe, amesema aliona mauzauza kwenye mabao matatu aliyofungwa na Simba, juzi. Simba ilitoka nyuma na kufanikiwa kushinda kwa mabao 3-2 dhidi ya Mbao ya Mwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Katika mchezo huo hadi dakika ya 80 Simba walikuwa nyuma kwa mabao 2-0, lakini wakaamka na kufanikiwa kupata ushindi huo uliowaepeleka kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuwa na pointi 58, mbili mbele ya Yanga wenye pointi 56.
Ngwengwe ambaye kabla ya kufung-wa mabao hayo alikuwa ameonyesha ki-wango cha hali ya juu, aliliambia Cham-pioni Jumatano kuwa, mabao hayo hayakuwa ya kawaida.
Kipa huyo amesema kuanza bao la kwanza lililofungwa na Frederic Blag-non hadi la mwisho la Mzamiru Yassin alikuwa hauoni mpira. “Kwa namna mabao yalivyokuwa ya- naingia hata watu waliokuwepo uwan-jani naamini walikuwa wanashangaa lakini ukweli ni kwamba kulikuwa na mauzauza japo mtu wa kawaida hawe- zi kuelewa wala kuamini hali ambayo nilikuwa naiona pale uwanjani.
“Kweli nimeumia sana kwa matokeo tuliyoyapata dhidi ya Simba kwani tuli-kuwa mbele kwa bao 2-0 lakini kipindi
cha pili hasa dakika za mwisho nilian- za kuona mauzauza kila ninapotaka kushika mpira hata zile bao ukiangalia
zimefungwa katika mazingira ambayo mtu wa kawaida hawezi kuamini,” alisema Ngwengwe
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka