KUWA MAKINI , HII APA STAILI MPYA YA UPORAJI WA PIKIPIKI | BONGOJAMII

KUWA MAKINI , HII APA STAILI MPYA YA UPORAJI WA PIKIPIKI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
STAILI mpya ya uporaji pikipiki imeanza kuutikisa mkoa wa Kilimanjaro, ambapo watu wasiojulikana hutumia usafiri wa magari kusimamisha madereva wa vyombo hivyo barabarani na kisha kupora na kutokomea.

Akizungumza mjini hapa jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah, alisema katika moja ya matukio hayo, mkazi wa Maili Sita, Haji Hassan (40) aliporwa pikipiki aina ya Boxer na kujeruhiwa kwa shoka baada ya watu wasiojulikana wakiwa na gari kumsimisha kama wanataka msaada na kuporwa pikipiki.

“Natoa wito kwa madereva wa pikipiki kuchukua tahadhari kutokana na mbinu hii mpya ambayo inaanza kujitokeza kwa watu kujifanya kama wanahitaji msaada wa kuharibikiwa gari ama kuishiwa mafuta lakini kumbe lengo lao ni kupora pikipiki,” alisema.

Akizungumzia mkasa uliomkuta, Hassan alisema watu hao walimsimamisha kama wanaomba msaada na aliposimama, ghafla walitokea watu wengine wawili nyuma yake na kumvamia na kumjeruhi kwa shoka mguuni na mkononi na kumpora pikipiki yake.

Alisema tukio hilo lilitokea Aprili 18, mwaka huu, majira ya saa 19:30 usiku, katika eneo la Sango, kata ya Msaranga, Manispaa ya Moshi.

Alisema pikipiki iliyoporwa ina namba za usajili 451 AUJ yenye thamani ya Sh. milioni mbili ambayo alikuwa akiiendesha akitokea kijiji cha Ngage, wilaya ya Mwanga kuelekea Maili Sita.

Tukio jingine lililozusha taharuki lilitokea wiki iliyopita katika mji mdogo wa Sanya Juu, wilaya ya Siha, baada ya kuuawa dereva wa bodaboda na kuporwa pikipiki aina ya Boxer na kisha mwili wake kutupwa kwenye shamba la mahindi kijiji cha Kilingi.

Aliyeuawa ametajwa kuwa ni Peter Godlove, ambaye inadaiwa kabla ya tukio hilo alikodishwa na mtu asiyemfahamu majira ya saa 2:10 usiku eneo la Sanya Juu na baada ya kuondoka hakurejea tena hadi alipookotwa amekufa.

Featured Posts