Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Nuh Mziwanda amesema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema aliingia kwenye mahusiano mapya kipindi ambacho tayari alikuwa ameanza kuona mwanga kwenye muziki wake lakini mapenzi hayo yalimfanya kuridhika na kujikuta anashindwa kukaza tena kwenye muziki.
"Mimi nakumbuka mahusiano yangu ya nyuma yalinirudisha nyuma sana kimuziki, yaani nili relax sana. Nakumbuka wakati naanza mahusiano hayo nilikuwa nimeachia wimbo wangu wa 'Otea nani' ambao ulikuwa unanipeleka sehemu nzuri kimuziki lakini ile njaa niliyokuwa nayo kwenye muziki ya kutaka kutoka nilivyokutana na hayo mahusiano mapya nikalegeza, nika relax mwenyewe najua kitu fulani nimepata lakini kumbe ni utoto hivyo nimejifunza sema huwa najutia kupoteza ule muda" alisema Nuh Mziwanda
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka