MARUFUKU KUDAI KODI KWA BUNDUKI.....RC MRISHO GAMBO AFUNGUKA | BONGOJAMII

MARUFUKU KUDAI KODI KWA BUNDUKI.....RC MRISHO GAMBO AFUNGUKA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Kufuatia taharuki iliyokuwa imetanda katika jumuiya ya wafanyabiashara mkoani Arusha dhidi ya zoezi la ukusanyaji kodi linalo endeshwa na mamlaka ya mapato nchini TRA, mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amepiga marufuku zoezi hilo kufanyika likiwahusisha askari wenye mitutu ya bunduki na badala yake zoezi hilo lifanyike kwa kufuata misingi ya sheria zilizopo na utu ndani yake.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Arusha Walter Maeda anesema kutokana na vitisho vingi kutoka kwa baadhi ya maafisa wa TRA na askari waliokuwa wakiambatana nao wakati wa zoezi la kukusanya kodi,baadhi ya wafanya biashara walifikia uamuzi wa kufunga biashara zao na wengine hata kufikiria kuhamisha biashara zao.

Kufuatia hali hii mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo anaamua kuingilia kati na kusema ni lazima zoezi hilo liwe na chembe za utu ndani yake kwa kuzingatia sekta binafsi ni muhimu katika uchumi wa mkoa wake na taifa kwa ujumla na hapa anatoa maelekezo.

Meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Arusha Apili Mbaruku anasema katika zoezi hilo askari walitumika kwa nia njema ya kuimarisha usalama lakini wapo waliokiuka maelekezo na kuamua kufanya yao na kwa maana hiyo kuanzia sasa hakutakuwa na askari tena katika zoezi la ukusanyaji kodi ya mapato.

Baada ya maekezo hayo wafanya biashara wanamshukuru mkuu wa mkoa huyu kwa uamuzi alioufikia huku wakiainisha baadhi ya changamoto zingine.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts